mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Mtu mmoja anaefahamika kwa jina la Meshack Azikam (23) mkazi wa mtaa Kichangani Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa kosa la kuiba misalaba 14 katika makaburi ya Kola.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro ACP Alex Mkama amesema, jeshi hilo lilipokea malalamiko kuwepo kwa wizi wa misalaba ndipo walipofanya msako na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye ni fundi seremala ambaye anatumia misalaba hiyo kama vyuma chakavu.