Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Masoud, amesema chama hicho kina taarifa na ushahidi wa awali unaojumuisha picha, video, mawasiliano pamoja na miamala ya fedha inayodaiwa kutumwa kutoka kwa wanachama wa kile alichokiita "chama cha kikaragosi" kwenda kwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA.
Amesema ushahidi huo umekabidhiwa kwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kwa ajili ya uchambuzi na hatua za kisheria, akidai kuwa baadhi ya viongozi wa majimbo, hususan mkoani Morogoro, walipigiwa simu na wengine walipokea fedha lakini hawakuitikia wito huo.