Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Paullih

Member
Joined
May 12, 2008
Posts
85
Reaction score
15
Hivi umepata kujiuliza unapopita katika mitaa mbalimbali ya mjini Dar au mji mwingine wowote Tanzania, jina la mtaa au eneo husika limetokana na nini?

Kwa mfano, Kijito Nyama limetokana na nini? Au Mlalakuwa, Au Mtoni kwa Aziz Ali n.k, n.k. Labda utadhani imetokea tu ... just ipo ipo, hapana! Baadhi ya majina ya mitaa yana historia ndefu na yenye kukumbukwa hata kwa vizazi vijavyo.

Hapa napenda kuwahabarisha maana ya mtaa au eneo la nje kidogo ya jiji la Dar liitwalo Gongo la Mboto.Jina hili limetokana na nini? Nakumbuka nilipata kusimuliwa na mwalimu wangu mmoja miaka ile pale Tambaza Sekondari nikiwa kidato cha pili.

Alisema palikuwa na mzee mmoja mashuhuri ambaye alipata kuishi katika eneo hilo.Huyu jamaa alikuwa mkulima. Jina lake aliitwa Mboto. Siku moja alijilawa kwenda katika konde lake kwa ajili ya kujipatia riziki.

Wakati ule, maeneo yale yalikuwa na giza la mapori na vichaka kadhaa. Jioni yake asirudi nyumbani. Kesho yake hadi mchana Mboto haonekani.

Mbiu ikapigwa watu wakakusanyika,kilichofuata ni msako mkali wa kumtafuta mzee huyu.Baada ya siku kadhaa wakakuta nyayo za mnyama mkubwa mithili ya Simba na ishara ya purukushani kadhaa.

Walipochunguza zaidi wakafanikiwa kukuta Gongo ambalo alipenda kutembea nalo mzee huyu.Wakahisi kuwa Mboto huenda amekutwa na maafa ya kuliwa na Simba. Walichokiona pale ni Gongo lake,Ndipo hilo eneo hadi leo lajulikana kama Gongo la Mboto.

Tuhabarishane maana ya maneno mengine kama Msasani, Mikocheni,Mto wa Mbu n.k.



 
Chekelei - Check the Railway
Chekereni - Check the Train
Kariakoo - Carrier Crops (?)
Kilimanjaro - Kilima Kyaro (?)
Lugalo - Alipopigwa Jerumani Emily Von Zelewisky na Jeshi la Mkwawa
Same - Mzungu kila akienda hapo alikuwa anaona kile kitu kiko vilevile (?)
Simba - Kuna mtu aliliwa na simba katika hiyo barabara pale Chuo Kikuu
 
Hapo kitambo mitaa ya MwanaNyamala kulikuwa na mapori na wakabaji, kwa hiyo kina mama wa kizaramo walivyokuwa wakifika mitaa hiyo wakawa wanawaambia watoto wao "Mwana Nyamala" maana yake "Mtoto Nyamaza" ili wasisikiwe na maharamia.

Kijito Nyama inawezekana ina uhusiano na Mwana Nyamala, kwamba unavuka kijito ukifika upande wa pili huko "Mwana nyamala" Nyamaa == Kijito Nyamaa mwisho ikawa Kijitonyama.

Mtoni kwa Aziz Ali pamepata jina kutokana na mkazi mmoja alwatani sana marehemu Aziz Ali. Mzee huyu alifariki miaka kadhaa iliyopita kukawa na kesi kubwa sana ya urithi kati ya wanawe.
 
Wana JF,
Ningependa kujua maana na asili ya majina ya sehemu mbalimbali za nchi yangu Tanzania (just curiosity)….
1. Tanganyika
2. Zanzibar
3. Dar es Salaam (bandari ya salama?)
4. Morogoro/Kilimanjaro/Ruvuma/Tanga na mikoa mingine
5. Pemba/Unguja/Mafia na visiwa vingine
6. Ilala/Temeke/Kinondoni na wilaya nyingine
Kama kuna anayejua asili/maana ya jina la sehemu hizo (ama nyingine) naomba atoe darsa hapa.

 
Bagamayo = Bwaga moyo yaani tua moyo....
Moshi ina uhusiano na moshi utakanao na kuungua kitu?
 
Kariakoo ilitokana na sentensi ya kizungu enzi hizo. Pale ilikuwa nisehemu ya kufanyia manunuzi ya bidhaa toka kwa wakulima.Kumbuka wakulima wa pwani hawakuruhusiwa kuvuka Anatoglo. Hivyo vijakazi wa wazungu na wahindi walitumwa pale ilipo kariakoo kuchukua/kununua bidhaa za shambani Ikawa CARRY AND GO, waswahili wakashindwa kutamka maneno hayo vizuri basi wakaishia kusema kariakoo badala ya carry and go. Sehemu kabla ya kubadilishwa wenyewe waliita tua tugawane. Kama kuna historia sahihi basi iletwe hapa.
 

Jina Kariakoo lilianza tokea enzi kabla ya mjerumani, kijiji hiki kiliitwa "Carrier Corps." Hii sehemu ilipata umaarufu sana kwa sababu ilikuwa frequently raided by slave masters kuja kuchukua watumwa. Kwa mantiki hii, jina halisi ni Carrier Corps ila wenyeji walitamka walivyoweza, hence, Kariakoo.
 

Wakati wa vita vikuu vya pili, katika sehemu inayoitwa sasa Kariakoo, kulikuwa na kambi kikosi cha mizigo ya jeshi la wakati huo, Kings African Rifkes (KAR) na kikosi hicho kilikuwa kinaitwa Carrier Corps. Kwa sababu Waswahili walishindwa kutamka matamshi hayo, walipaita Karia Koo!!
 
Singida- mapambo ya kuvaa masikioni kama hereni; wazungu wakiwauliza babu zetu nini hiyo waliwajibu Singida. Basi ikawa SINGIDA!
 
Dar es salaam imetokana na neno Daru salaam,kwa maana ni mji wa amani na sio bandari salama.

I doubt if this history is correct. Is 'Daru salaam' also arabic? Dar es Salaam is arabic for a safe habour Bandari (dar) ya(es) Salama (Salaam). By then most of the hobours along the indian coast were not safe for arab merchants.
 
Kuna mwenyeji mmoja wa Kigoma aliwahi kuniambia kuwa ktkt ziwa Tanganyika kuna samaki wawili mashuhuri sana ambao kwa kiha wanaitwa "Itanga" na "Nyika". Mmoja wao inasemekana ana umeme mkali.

K/hiyo, huenda neno "Tanganyika" limetokana na majina ya samaki hao.

Labda Mh. Zitto Kabwe anaweza kutueleza zaidi.
 
Dodoma:- Kuna tembo alienda kunywa maji na akazama. Sehemu hiyo alipozama tembo wakaiita IDODOMYA. Hiyo ikaja pelekea jina Dodoma.
Msasani :- Kwa Musa Hasaan. Wamakonde wakasema "Kwa Ncha-Chani". Wakuja kama sisi tukajua ni Nsasani au Msasani. Hivyo wakarebekisha makosa ya Makonde na ikawa Msasani.
Tabora:- Kambi ya Wafanyabiasha. Walikuwa wakipita na bidhaa zao wanakuta viazi vitamu vilivyopikwa na kukatwakatwa vipande na kuanikwa. Hapo huliwa makavu (Chewing gum) au kupikwa na kuliwa. Haya huitwa Matobolwa au Matovola. Hivyo wakapaita kambi ya Matobolwa au Matovolwa. Hii ilikuwa kugeuka na kuwa Tabora.
Bagamoyo:- Bwaga Moyo. Ukifika hapo ujuwe umeshakuwa mtumwa, no escape.
 
Kilimanjaro
Kwamba wazungu walipouliza jina la ule mlima wachaga wakasema Kilelema kyaro (maana yake kilichoshinda wengi), wazungu wakaandika Kilimanjaro... (Hii naomba kama kuna mtu anaweza kuthibitisha.
Manyara
Inatokana na minyaa?

BOMA
British Overseas Management Administration (hii niliipata kwa bwana mmoja wa makumbusho ya pale BwagaMoyo)

BTW: Nitaanza kuiita Carrier Corps badala ya Kariakoo....asante Kisura na Kitia ila historia mlizotoa zinatofautiana. But thanx.
 

BTW: Nitaanza kuiita Carrier Corps badala ya Kariakoo....asante Kisura na Kitia ila historia mlizotoa zinatofautiana. But thanx.

Historia ya Carrier Corps ilianza kabla ya mkoloni kuweka military base pale, hii ilikuwa baadae sana.

Kama nilipoeleza juu, kijiji kilianza kwa kuwa raided, watumwa/wabebaji wa mizigo hiyo waliitwa "carriers" au wabeba maboksi na mabwana zao. Wenyeji wa pale walikuwa wakibeba mizigo ya masters bure kama watumwa na kabla ya kusafirishwa kuja Amerika, ingawa baadae kidogo wakaanza kulipwa. Baadae, Kariakoo ilitumika kama military depot. Historia ya jina imeanza kwa watumwa kabla ya uhifadhi wa silaha.
 
Sumbawanga- Wenyeji wa maeneo hayo walikerwa na vitendo vya ushirikina (tofauti na mtazamo wa watu wengi kwamba wenyeji wanaendekeza ushirikina). Kutokana na kero hiyo waliamua kuwapiga mkwara watu wanaoingia katika mji huo kwamba kama unataka kuja huku, basi Tupa Uchawi i.e Sumba (Tupa) Wanga (Uchawi), ukitupa na kuuacha uchawi wako huko uliko unaruhusiwa kuja hapo Sumbawanga !!!
 

Roy,
Asante kwa neno BOMA. Nilikuwa sifikirii kuwa ni neno la kizungu. Utasikia hata zizi wengine husema BOMA la Ng'ombe.

SERENGETI:- Ni Ardhi isiyo na mwisho (Endless land). Wamasaai walitembea na mifugo yao bila ya kufika mwisho. Hivyo wakaiita hiyo Mbunga Serengeti.
 
Kijiji cha Chekeleni.

Kuna reli imepita katikati ya barabara baada ya Mombo kupita kama unaelekea Moshi. Kuna kijiji kinaitwa Chekeleni sehemu hiyo. Historia ya jina ni kuwa, kuna reli ina pita pale katikati ya barabara, sasa kiliwekwa kibao kinasema Check Rail , ila ndugu zetu iliwawia ugumu pale, wakaja na Chekeleni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…