1 Nimesikia baadhi ya watu kusema Mlima Kilimanjaro ni jina la kizungu (wageni). Naomba niwaelimishe kwa sehemu tu. Jina la Mlima Kilimanjaro lilitokana na neno la kichaga lililosema - Kilema Kyarwa ikimaanisha Mlima wa Ajabu/ Mlima wa Mungu, kutokana na Volikano iliyo kuwa inatoka. hayo mapokeo wageni walishindwa kuyatamka vema na kuanza kuita Kilimanjaro.
2 Asili ya jina Mbeya wengine husema wahindi walishindwa kusema neno chunvi kwa kisafwa yaani Iv'eya. Mimi nasema asili ya jina la Mbeya ilitokana na chifu aliyewahi kutawala eneo hilo ambaye aliitwa chifu Mbeye, katika kutamka waka wageni wanaanza kuingia kwenye nchi ya chifu Mbeye ndio wakaanza kusema Mbeya mpaka leo. Lakini binafsi sijajua mpaka leo kaburi la huyo chifu alizikwa wapi au ndiyo huko mbeya mlimani sijui. hebu nipanueni hapo.
3 Kwa kifupi tu Mama John amezalisha majina yafuatayo jiji la Mbeya:- Sinde, Makungulu, Mwanjerwa, na Mama John. = Makungulu ndipo alipokuwa anaishi alitunza miti ambayo kungulu walikuwa wanalala kwa wingi. Sinde - aliweka kilabu cha pombe ya kienyeji na wateja wake walikuwa wanakaa kwenye vitita vya nyasi kama viti kwa kisafwa vitata hivyo vinaitwa INSINDE. mji ulipoanza kupanuka kilabu hicho kilipitiwa na ramani ya barabara ya sokomatola mwanjelwa na kumsababishia kuhamisha kilabu hicho eneo jipya yaani MAMA JOHN - mpakaleo hiyo mama John. na mwanae aliyeitwa jina lake Mwanjelwa ndiye alijenga nyumba yake hapo mwanjelwa na baadaye eneo hilo likabaki kwa jina la Mwanaye MWANJELWA mpaka leo. Karibuni wana historia kudadavua