Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Ulipotelea wapi wewe
 
TABATA😛alikua na mwarabu eneo hilo alikua anadaiwa wenye hela yao wakimfata anawajibu UTAPATA ,Kwakua lafdhi yaki arabu iana mushkel kwenya U na P akawa anatamka TABATA
Hakuwa mwarabu, ni muhindi alikuwa na duka la jumla la kuuza nafaka. Makuli waliokuwa wakimshushia mzigo baada ya kazi na kuomba pesa akawa anawajibu utapata ila kwa lafudhi ya kihindi ndio ikawa inasound "Tabata" taratibu hilo jina likashika.
 
Sea breeze= Chibirizi (Kigoma)

Ila samahani mleta mada kuna majina huku Manyara yanaishia na consonant sijui chanzo chake mf. Katesh, Hanang, Endabash, Endasaq,
Mkuu umenikumbusha mbali, nilikuwa huko mwezi wa 8 kuna jamaa angu ame settle kule!
 
nilivo sikia ni kwamba apo simu 2000 kulikuwa na wizi mkubwa wa simu na ilibiwa kwa muda huo na kuuzwa muda huo kwa bei ya chini kabisa 2000 ndo leo panaitwa ivo simu 2000
Duh asante kwa ku clear doubt yangu ya mda mrefu. Nilikuwa nikihisi maana ya simu 2000 ni kama ulivyoeleza kuwa wazee wa Ndolema walikuwa wakizipiga simu wanaziuza buku 2
 
Wareno walileta zao la korosho ktk maeneo ya mwambao wa Bahari ya Hindi mnamo karne ya 16. Maeneo yanayostawi korosho ni Mtwara, Lindi, Mafia, Bagamoyo, Rufiji na kwa mbali kidogo mkoa wa Tanga.

Kwa lugha ya kireno, korosho uitwa Castanha de Caju, kwa kifupi de caju.
Wadigo wa Tanga hawakuweza kutamka neno de caju, wao walitamka mi kaju au mi kanju.
Eneo lililostawi mikorosho liliitwa Mikajuni au Mikanjuni.
Mkorosho = Mkaju/Mkanju.
 
Msasani Kulikuwa Na Mzee Mmoja maarufu akiitwa Musa Hasani, Hivyo Pakaitwa Mtaa Wa Musahasani Wabongo Wakasimplify ' Msasani'
Wamakonde ndio waliotamka hivyo kutokana na lafudhi yao
 
Kawe- Cowway [emoji230]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wakuu katika pitapita zangu nimekutana na historia ya majina ya sehemu ambayo yanatumika hivi sasa kutoka kwenye maneo ya kiingereza;
Do me Love = Dumila (Morogoro)
Mind You = Mindu (Morogoro)
Kill bad Guy = Kibaigwa (Dodoma)
Guy Love = Gairo ( Moro)
Man and Tom Boy = Matombo (Morogoro)
If I care her = Ifakara (Moro)
New Alert = Newala (Mtwara)
Carrier Corps = Kariakoo (Dsm)
Kill it Off Site = Kilosa (Moro)
Kill it on Bed or Down = Kilombero (Moro)

Wakuu mnaweza ongezea karibuni.....
 
Tafuta uzi mmoja hivi uliwekwa na Kanungila Karim ulikuwa unaelezea asili na jinsi jina la IFAKARA lilivyotokea.
Hapo ulipoandika umeandika upupu tupu
 
kabla ya mjerumani unamaanisha toka kipindi cha ujio wa waarabu na waarabu hawakuzungumza kiingereza na ili jina "Carrier Corps." linaasili ya kiingeleza ilikuaje lianze jina la kiingereza kabla ya ujio wao???
 
mikanjuni ni mjini hasa hakuna hata korosho moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…