Kuna mwenyeji mmoja wa Kigoma aliwahi kuniambia kuwa ktkt ziwa Tanganyika kuna samaki wawili mashuhuri sana ambao kwa kiha wanaitwa "Itanga" na "Nyika". Mmoja wao inasemekana ana umeme mkali.
K/hiyo, huenda neno "Tanganyika" limetokana na majina ya samaki hao.
Labda Mh. Zitto Kabwe anaweza kutueleza zaidi.
The name 'Tanganyika' is derived from the Swahili words tanga meaning 'sail' and nyika meaning an 'uninhabited plain' or 'wilderness'. At its simplest it might therefore be understood as a description of the lake 'sail in the wilderness'.
Mkuu Tz1,
Niliwahi kusikia historia hii ya jina Tanganyika (ziwa) kuhusishwa na samaki, lakini pia kuna wengine wanahusisha na maneno mawili ya TANGA na NYIKA.......
Je, inamaanisha kwamba nchi ya Tanganyika ilitohoa jina lake ziwa Tanganyika?
Kuna maelezo wikipedia ambayo hayaniingia sana akilini
Moshi check rail kwenye rail cross wakapaita chekereni.
Kilimanjaro = Mlima cha Mungu kama ilivyo Oldonyo lengai?
Moshi = ni Kijerumani Moschee = Msikiti
Arusha = Kimaasai La- Arusha = ng'ombe kijivu
Karatu = Kiyunani (the name of settler) (kratoo maana yake kutamalaki, kutawala)
Kuna mwenyeji mmoja wa Kigoma aliwahi kuniambia kuwa ktkt ziwa Tanganyika kuna samaki wawili mashuhuri sana ambao kwa kiha wanaitwa "Itanga" na "Nyika". Mmoja wao inasemekana ana umeme mkali.
Roy,
Asante kwa neno BOMA. Nilikuwa sifikirii kuwa ni neno la kizungu. Utasikia hata zizi wengine husema BOMA la Ng'ombe.
SERENGETI:- Ni Ardhi isiyo na mwisho (Endless land). Wamasaai walitembea na mifugo yao bila ya kufika mwisho. Hivyo wakaiita hiyo Mbunga Serengeti.
Kwa historia niliyoisoma, Jina Dar Es Salaam limebadilishwa ile "EL" na kuwekwa "ES". Jina halisi laKiarabu lilikuwa Dar El Salaam, likiwa na maana ya Bandari salama.
Kijiji cha Chekeleni.
Kuna reli imepita katikati ya barabara baada ya Mombo kupita kama unaelekea Moshi. Kuna kijiji kinaitwa Chekeleni sehemu hiyo. Historia ya jina ni kuwa, kuna reli ina pita pale katikati ya barabara, sasa kiliwekwa kibao kinasema Check Rail , ila ndugu zetu iliwawia ugumu pale, wakaja na Chekeleni!
Kiambata "al" ktk Kiarabu (ambacho wkt mwingine hutamkwa el) ni sawa na definite article "the" ktk Kiingereza. Kuna baadhi ya herufi, kutokana na ugumu wake kimatamshi, hazikubali kiambata hiki ("al") km kilivyo. "Al" ikikutana na herufi hizo, herufi yake "l" huondolewa, na "a" iliyobakia huunganishwa na herufi ya kwanza ya neno linalofuata, huku herufi hiyo ikiwekewa uzito (kwa kufanywa double). Kwa mfano, herufi "s" ya kiarabu haikubali kutanguliwa na "al". Kwahiyo, neno lolote la kiarabu linaloanza kwa herufi "s" likitanguliwa na kiambata "al", basi herufi "l" ya "al" huondolewa, na "a" iliyobakia huunganishwa na "s" mbili. Hivyo, al salaam huwa assalaam -- Km ktk Assalaamu Alaykum - (The) Peace (of God) be upon you.
K/hiyo, Dar El Salaam, kutokana na kanuni zilizoelezwa hapo juu, si sahihi; bali Dar Es Salaam (kutokana na Kiarabu Daru Ssalaam -- badala ya Daru El Salaam) ndilo neno sahihi.
Kijiji cha Chekeleni.
Kuna reli imepita katikati ya barabara baada ya Mombo kupita kama unaelekea Moshi. Kuna kijiji kinaitwa Chekeleni sehemu hiyo. Historia ya jina ni kuwa, kuna reli ina pita pale katikati ya barabara, sasa kiliwekwa kibao kinasema Check Rail , ila ndugu zetu iliwawia ugumu pale, wakaja na Chekeleni!
Kilimanjaro
Kwamba wazungu walipouliza jina la ule mlima wachaga wakasema Kilelema kyaro (maana yake kilichoshinda wengi), wazungu wakaandika Kilimanjaro... (Hii naomba kama kuna mtu anaweza kuthibitisha.Manyara
Inatokana na minyaa?
BOMA
British Overseas Management Administration (hii niliipata kwa bwana mmoja wa makumbusho ya pale BwagaMoyo)
BTW: Nitaanza kuiita Carrier Corps badala ya Kariakoo....asante Kisura na Kitia ila historia mlizotoa zinatofautiana. But thanx.