Amaan ameshawahi kupelekwa Malawi akiwa mdogo
Malawi kuna makabila mengi, sasa jina KARUME linapatikana katika kabila lipi katika hayo makabila ya huko??, isitoshe Malawi katika zama hizo kupata Muisilamu ilikuwa ni shida kubwa, "Abeid na Amani" hayo majina mawili yana asili kiarabu na yapo sana miongoni mwa Waisilamu.
Angalia majina (surnames) za Wamanyema (Wabwali, wanyakaramba na Wagoma):-
Kaluona, Kainuza. Kasanga, kairo,Kafungo, Kaluta, kazema,Kakolwa, Karume, kaila, nk japo yapo majina Mengine ya hayo makabila hayaanzi na silabi "Ka" lakini mengi yanaanza na "ka".
Kama nilivyosema hapo awali Wamanyema walitoka Kongo DRC zamani na wakaingia Kigoma na kiasi fulani Kagera, Rukwa na Tabora, idadi yao kubwa ilifika hadi Dar na wachache wakaingia Unguja. Ni vigumu sana kumpata mmanyema asiyekuwa Muisilamu ila wapo wasiokuwa waisilamu ila ni wachache sana, mfano Ujiji inao wamanyema wengi idadi yao kubwa ni Waisilamu na huko majina ya Karume yametamalaki hadi hii leo.
Ndiyo maana nasema, Marehemu Abeid Amani Karume ni "Mmanyema", hata nilipata kumsikia Dr Salim Ahmed Salim akihojiwa na akasema (kama nakumbuka vyema) yeye DR, anayo damu ya kimanyema katika "Geneology" yake kuna mzazi wake mmoja ni mmanyema, hii maana yake ni kwamba Wamanyema kama ilivyokuwa kwa makabila mengine kama wasukuma na Wanyamwezi waliingia Unguja zamani sana kutoka Tz Bara, kama ilivyo kwa Wadigo walivyoingia Pemba kutoka Tanga.
Au vinginevyo atakuwa na asili ya Mmanyema aliyeingia Malawi kutoka Congo DRC.
that's my take.