View attachment 3226411
Fundi cherehani wa kwanza wa Kihindi huko Kisumu- Kenya mnamo 1890 ambaye alianzisha Mashine ya Kushona, jina lake lilikuwa
Charan Singh .
Wajaluo waliamua kuiita mashine hiyo
CHARAN.
Waganda walilikubali jina hilo na kuliita
EKYALAANI.
Waswahili pia wanaita “
CHEREHANI” hadi leo..
Zamani Wahehe walikuwa Wanaitwa Wana-Mtwa.
Walipokiwa wakipigana na wajerumani huku wao wakitumia mishale na mikuki, wajerumani wakitumia bunduki, ikawa wajerumani wakifyatua risasi, wenyewe wanajikunga na ngao. Wakawa wanashaa inakuwaje tunajikinga lakini tunskuwa. Katika kushangaa wakawa wana "He he" kila wenzao wakidondoka wanasema "He hee" huku wanakimbia.
Kuanzia siku hiyo wakaitwa "Wahehe"
×××××××××××××××××××××××××××××××××
Kuna siku maeneo ya Tukuyu , ilikuwa mwaka 1901 alikuja mzungu na baiskeli yake. Watu wakakusanyika kumshangaa anavyoiendesha.
Akauliza kama kuna yeyote kati yetu anaweza kuendesha ampe ajaribu. Akajitokeza mmoja wetu, tukapinga sana kwamba hawezi, yule mzungu akasema muacheni ajaribu, basi jamaa alipopewa, kwa maajabu tukashangaa anaendesha.
Ndipo yule mzungu akauliza, mlikuwa mnamcheka si mmeona? Sisi tukskubali yaishe, tukasema "Basi kweli kaweza".
Jamaa akawa akitutambishia sana, hata tukiwa na story nyingine yeye anatumbukizia za kuendesha kile chombo, sisi tukawa tunamjibu "basi kweli".
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa jina baiskeli.
Zingatia: Mwaka ni 1901