Asili ya jina la msaidizi wa dereva kuitwa "TANDIBOI" πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Katika kipindi cha kabla ya enzi ya ukoloni, na hata ukoloni ulipoingia nchini Tanganyika, aina hiyo ya magari ndio yalikuwa vyombo vikuu vya usafiri nchini.

Magari hayo hayakuwa ya kuwasha kwa funguo (ignition key/starter). Yaani yalikuwa yanawashwa kwa kuzungusha "hendeli" kwa mikono.πŸ˜€

Ukiangalia kwa makini ama ukizoom, unaweza kuona kuna kimtalimbo ambacho kimechomoza kwa mbele, chini kidogo ya taa. Kwa hivyo ili kuwasha injini ilibidi uzungushe hio hendeli kwa dakika kadhaa, kama wafanyavyo wasaga unga katika mashine za kusagia za kizamani.

Wakati hio kilikuwa na vijana wa kiume wenye msuli kidogo ambao ndio waliokuwa wakifanya kazi hiyo.

Na dereva, aghalabu alikuwa mzungu, akishaingia ndani ya gari alikuwa anampigia kelele kijana wa kuwasha gari: "OK! Turn Boy! turn boooy!! Yaani zungusha (hendeli) kijana! Zungusha kijana.

Nasi Wamatumbi kama ilivyo kawaida yetu tukisikia neno lazima tulitohoe kivyetu. Hivyo hata baada ya magari ya kuwashwa kwa hendeli yalipotoweka na kuja ya kuwasha kwa funguo, hadi leo msaidizi yeyote wa dereva, hasa wa lori, anaitwa "Tandiboi" ikimaanisha "Turn boy.... πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Hiyo
Screenshot_20240916-103322.png
 
Hv turn boy ndio conductor?
Turn boy kwenye gari au basi au semi au lorry ni fundi na msaidizi wa dereva kwenye swala zima la mizigo. Conductor ni yule anayesimamia mapato na abiria kwenye gari. Bus zina conductor dereva na turn boy au kiboot yule anayefungua mabuti na kupakia mizigo pia gari ikipata itilafu ndo utawakuta wameshikilia spana.
 
As
Katika kipindi cha kabla ya enzi ya ukoloni, na hata ukoloni ulipoingia nchini Tanganyika, aina hiyo ya magari ndio yalikuwa vyombo vikuu vya usafiri nchini.

Magari hayo hayakuwa ya kuwasha kwa funguo (ignition key/starter). Yaani yalikuwa yanawashwa kwa kuzungusha "hendeli" kwa mikono....πŸ˜€

Ukiangalia kwa makini ama ukizoom, unaweza kuona kuna kimtalimbo ambacho kimechomoza kwa mbele, chini kidogo ya taa. Kwa hivyo ili kuwasha injini ilibidi uzungushe hio hendeli kwa dakika kadhaa, kama wafanyavyo wasaga unga katika mashine za kusagia za kizamani.

Wakati hio kilikuwa na vijana wa kiume wenye msuli kidogo ambao ndio waliokuwa wakifanya kazi hiyo.

Na dereva, aghalabu alikuwa mzungu, akishaingia ndani ya gari alikuwa anampigia kelele kijana wa kuwasha gari: "OK! Turn Boy! turn boooy!! Yaani zungusha (hendeli) kijana! Zungusha kijana.

Nasi Wamatumbi kama ilivyo kawaida yetu tukisikia neno lazima tulitohoe kivyetu. Hivyo hata baada ya magari ya kuwashwa kwa hendeli yalipotoweka na kuja ya kuwasha kwa funguo, hadi leo msaidizi yeyote wa dereva, hasa wa lori, anaitwa "Tandiboi" ikimaanisha "Turn boy.... πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Aseh..ndo nimekuja kujua Leo... ahsante sana
 
Kuna picha niliona pale NIT ikirembeshwa na hii story.
 
Back
Top Bottom