Asili ya jina Tanganyika

Asili ya jina Tanganyika

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
677
ASILI YA JINA TANGANYIKA.

Leo 20:30pm 15/06/2020

Ni furaha yetu sote kuwa tuliobarikiwa kuishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Sisi wananchi wengi na raia wa nchi hii tumeishi zaidi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili huru Tanganyika na Zanzibar,Leo niwaletee tafakuri jadidi iliyozaa jina Tanganyika ambalo baadae liliungana na Zanzibar kuizaa Tanzania tunayoishi hivi leo,Ungana nami kujua asili ya jina "Tanganyika".

Katika moja ya hotuba zake, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema "Hili jina la Tanganyika hata mimi sijui lililotokea wapi wala asili yake sijui ni nini! lakini ninajua Waingereza walilitoa mahali fulani"

Changamoto yetu ikaja kutafuta kwanini Tanzania bara kuliitwa Tanganyika ?
Sio kila kitu tumeze tu na wajukuu zetu kizazi cha tatu,nne hadi kumi tutawaelezea nini!?

Wengi tukarejea fasihi za Shabani Robert,mtu kama Marehemu Shabani Robert atakua alijua maana yake maana alikua ni mwana fasihi mtunzi wa vitabu na mjuzi wa lugha kweli kweli,kwake yeye kiswahili na lugha ilikuwa mahala pake,tulipokosa,tukasema tuwaulize wahenga watakua wanajua jina Tanganyika lilipotokea,na hili ndilo lilikuwa jibu,

Wazungu walipojigawia Bara la Afrika, Wajerumani na Waingereza wakapewa maeneo yaliyokuwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Walipofika hapo walikuta maeneo yenye tawala tofauti, watawala wakiwa na majina mbalimbali: Mwinyi, Mangi, Chifu, Sultan, n.k.

Ukanda wa pwani ulitawaliwa na waarabu kutoka Oman hivyo Wajerumani na Waingereza wakalipa fidia na kuwahamisha wamiliki.Wajerumani wakaliita eneo lao "Germany East Africa" nalo lilijumuisha Iliyokuwa Tanganyika, Rwanda na Burundi za leo.

Wajerumani waliweka makao yao makuu katika mji wa Tanga, na wakaugawa mji huo katika maeneo makuu matatu ya kiutawala:
Tanga mjini
Pangani, na
Wilhelm-Stahl (sasa inaitwa Lushoto).
Wajerumani walitamani wawe na jina rasmi la eneo lao walilogawiwa na wazungu wenzao, badala ya kuyaita Germany East Africa na Germany South West Africa (Namibia ya leo).

Inaaminika walianzisha juhudi hizo na kuzalisha jina, ambalo hata hivyo hawakuweza kulitumia.
Jina hilo lilipatikana kwa kuunganisha,TA kutoka Tanga
NGANI kutoka Pangani
STAHL kutoka Wilhelm-Stahl
Jina likawa TANGANISTAHL ambalo husomeka TANGANYISTA.

Bahati mbaya kabla ya jina kuzinduliwa dunia ikarindima kwa vita vya kwanza vya dunia, vilivyowaweka Wajerumani na Waturuki kwa upande mmoja na Waingereza na washirika wake upande wa pili,hadi mwaka 1919 makubaliano yalipofanyika pale Sommer Ubelgiji ya kuacha mapigano Wajerumani wakajikuta wanapoteza mali zao nyingi ulimwenguni.

Germany East Africa ikagawanywa kwa Waingereza na Wabelgiji na Germany South West Africa ikatwaliwa kinguvu na Makaburu wa Afrika Kusini.
Waingereza, waliopewa idhini na jukumu na League of Nations kuisimamia Germany East Africa, wakaingia kazini kupata jina jipya.
Kumbukumbu katika maktaba ya Jiji Dar es Salaam zinaonesha Waingereza walilipa eneo hili jina la Tanganyika.

Jina hili linanasibishwa na Mr. Parkinson aliyekuwa naibu gavana wa jimbo hilo.
Mr. Parkinson aliliwasilisha jina hilo kwa mabosi wake na rasmi lilianza kutumika February 1920.
Kwa jambo hilo Mr. Parkinson alitunukiwa cheo cha "Sir" na mtawala wa Uingereza, Malkia Elizabeth.

Hii ndio asili ya nchi hii kuitwa Tanganyika. Hili jina halikutokea tu hivi hivi, Shukrani ziende kwa Mhenga Bakar aliyetupatia dadavuzi hizi za kimkokotenge hata kupata tashwishi ya kujua asili ya jina letu la Tanganyika.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Kuna andiko lolote umesoma linaloeleza haya uliyoandika juu ya jina la Tanganyika?
Kuna ushahidi mahali unasomeka..jina Tanganyika linatokana na lugha ya kinyamwezi, kwamba wakoloni wa kijerumani wakiwa katika safari zao..na kumbuka eneo la Tabora ndio yalkuwa makao makuu ya utawala wa wajerumani kanda ya afrika mashariki ya wakati huo..wakoloni hawa walikuwa wakisafiri kwa miguu wakati huo pori kwa pori..kwa sababu za kutembea umbali mrefu na jua kali walihitaji maji ya kunywa..na hivyo walilazimika kuwauliza wenyeji wapi watapata maji ya kunywa..wanyamwezi waliwajibu UTANGE NYIKA MKUPANDIKA MINZE..wao walikariri maneno mawili ya mwanzo UTANGE NYIKA ambayo maana yake ni.. MKIVUKA HII NYIKA(Pori) MKUPANDIKA MINZE (mtapata maji) sasa kwa kulitamka wajerumani wakatamka TANGANYIKA..kwamba hii ni Tanganyika.. upo kijana???
 
hebu ngoja nianze kujifunza hii kitu maana sijui mimi, nimekua na nimekuta hili jina likiitwa hivyo
 
Back
Top Bottom