Sasha Fierce
JF-Expert Member
- Feb 7, 2009
- 361
- 5
SF,
Hii inatokana na kwamba - unapotanguliza shikamoo ni kama umeweka kizuizi cha heshima.Anapokataa kuitika inavyotakiwa ni kwamba alikuwa ana mpango mwingine na wewe na anashangaa barrier ya nini tena?
Ok kama hata alikuwa na mpango mwingine kwa nini asiitikie salamu yangu then akaendelea kutia hilo neno lake.Kwani akiitikia shikamoo yangu age yake itabadilika na kuwa young?.I think kuwa wazee wengine hawataki kuzeeka wanadhani bado wao ni vijana.
Kwanza how do you say shimakoo in english?labda ukisema hivyo mtu ataona humuoni yeye kama ni mzee.
With time hili neno litaachwa. Wengi wetu sasa hivi, hasa mijini ambako kuna wakazi 33% ya Watanzania, watu wanakwepa kutumia shikamoo maofisini; kuitoa au kuipokea. Wale ambao wamenizidi miaka 15 hawana tabu kuipokea, ila walionizidi miaka 10 hivi, wanaitikia japo kwa haya kiaina.
Nani ofisini kwao watu wanaendekeza shikamoo?
Habarini wana JF: Nimekuwa nikijiuliza sana tafsiri halisi ya maneno haya mawili Shikamoo na Marhaba. Na pia nataka kujua zaidi ya Tanzania ni nchi gani wanatumia aina hii ya salamu! NAWASILISHA.
kama hujui hata maana ya shikamoo na marahaba JF sio mahala pako. humu tunataka watu wenye uelewa na uwezo wa kupambanua mambo... hilo swali kamuulize mwalimu wako wa chekechea.....
wee hujui maana ya hayo maneno! bora uulize ueleweshwe kuliko kujifanya mjuaji!
kama hujui hata maana ya shikamoo na marahaba JF sio mahala pako. humu tunataka watu wenye uelewa na uwezo wa kupambanua mambo... hilo swali kamuulize mwalimu wako wa chekechea.....
jamani..........., nimemzodoa ACTIVISTA not otherwise!!Mkuu jamaa kauliza swali ingefaa zaidi umjibu kuliko kumzodoa kwani wewe ni sehemu ya the great thinkers
Marhaba...........inuka mtumwa wangu!
kama hujui hata maana ya shikamoo na marahaba JF sio mahala pako. humu tunataka watu wenye uelewa na uwezo wa kupambanua mambo... hilo swali kamuulize mwalimu wako wa chekechea.....
Mnajua lugha ya kiswahili ni mchanganyiko wa lugha nyingi na mtazamo wangu binafsi ni katika kiswahili Shikamoo na marahaba ni kitu kikubwa sana ambacho lugha nyingi hazina, kwani shikamoo ni ya mdogo to kumwamkia mkubwa (au mzazi) kwa heshima na taadhima zote! na mkubwa akiwa anaihitajia atakuambia hujambo?, nawe yabidi uitikie, sijambo shikamoo (baba, mama, babu, kaka, dada, shangazi nk)