Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijui kwa nini tunaitumia.Mi nadhani ukimwamkia mtu,habari yako! au habari ya saa hizi! Heshima haitapungua.
Nipo chini ya miguu yako?
Hayo ni maneno wameweka wazee wetu ili kupaka rangi shikamoo.
Mie naamini tafsiri yake ni hii
Shika=Shika
Moo=Kuna herufi moja mwanzo wameifuta.
OTIS
huo ni uhuni
Hapana, nilimsikia mzee mmoja TBC Taifa akifafanua maana na asili ya neno hili ni kumuamuru mkosaji akushike chini ya kikanyagio chako cha mguu ili umsamehe. Mfano umenitukana sasa ili nikusamehe nakuambila 'shikamoo' yaani uniguse sehemu ya chini ya mguu wangu na ntakuwa nimekusamehe.Ni sawa na kusema naomba baraka zako.....
Sikubaliani ASILAN na maelezo yako mkuu.Salamu si lazima iwe na maana sawa ni ile ambayo 'wewe' unategemea.
Mfano, lugha nyingi zina 'salamu' ambazo ukitafsiri maana yake utaishia kucheka. Lugha ni utamaduni..pia lugha ni kiashiria cha jinsi watu katika jamii husika wanavyofikiri.
Kwa maoni yangu Shikamoo ni nzuri sana..Waingereza 'hawana' salamu inayolingana uzito na shikamoo.
Mfano: Kwa Kiingereza utasikia mtu akiuliza, 'How old are you' = tafsiri ya neno-kwa-neno utasamaje?
Lugha si maneno pekee, ni jinsi watu tunavyofikiri.
Hapana, nilimsikia mzee mmoja TBC Taifa akifafanua maana na asili ya neno hili ni kumuamuru mkosaji akushike chini ya kikanyagio chako cha mguu ili umsamehe. Mfano umenitukana sasa ili nikusamehe nakuambila 'shikamoo' yaani uniguse sehemu ya chini ya mguu wangu na ntakuwa nimekusamehe.
Umeelewa sasa! Maana halisi ya SHIKAMOO si kusalimiana ila sisi tumeligeuza/chakachua kama kawaida yetu. Tuna salamu nyingi tu za kusabahiana na zenye heshima ila watunga vitabu vya kiswahili wamepotosha salamu hii.Mmmh naona pia haileti maana, saa nyingine unamwamkia mtu shikamoo humjui au hakujui sasa akusamehe kwalipi ulomkosea?
Kwa wenzetu wahindi anapokushika mguu ni sawa na kupata baraka kwa mtu aliyekuwa mkubwa kwako......so it makes sense!