Asili ya Mkoa Wa Shinyanga

Asili ya Mkoa Wa Shinyanga

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Mkoa umepakana upande wa kaskazini na mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera , upande wa kusini na Mkoa wa Tabora.
Mkoa wa Kigoma uko upande wa magharibi , na
mkoa wa Simiyu upande wa mashariki.

ASILI YA NENO "SHINYANGA"

Asili ya neno "Shinyanga" limetokana na neno IYANGA.
Iyanga ni mti uliokuwa unapatikana Shinyanga ambapo Mtemi wa Shinyanga wa wakati huo alikuwa anapenda kupumzika chini ya mti wa Iyanga kila siku jioni.
Baada ya ujio wa wakoloni walipouona mti huo walishindwa kutamka neno Iyanga na kumsema Shinyanga..
 
Masahihisho. Kulikuwa Na mganga maarufu akiitwa Inyanga. Kwa hiyo waliokuwa wanamtafuta wakawa wanaambiwa waende kwa Inyanga, ambapo kwa kisukuma eneo linaitwa "Chalo". Kwa hiyo wakawa wanasema "toleja ko Chalo sh'inyanga" yaani tunaenda kwa eneo la Inyanga, ndiyo ikawa Shinyanga.
Kwa maana hiyo neno Shinyanga Ni muunganiko wa maneno mawili; Sha/Shi kwa maana ya "cha/ya" Na Inyanga, yaani kwa Inyanga Na kwa maana hiyo hata utamkaji wa neno Shinyanga kwa Kiswahili Na Kisukuma/kinyamwezi Ni tofauti
 
Naona kichwa kingekuwa asili ya jina Shinyanga. Kama hapo ndio mada ilipoishia
 
Asili ya jina Shinyanga ni hii. Enzi za ukoloni eneo lote la Shinyanga ya sasa lilikuwa pori nene. Katika eneo ambalo leo linaitwa Old Shinyanga kulikuwa na mti mkubwa sana kuliko miti yote iliyokuwapo enzi hizo ambao ulijulikana kwa jina la "INYANGA" mti huu ulitumika kama ukumbi wa mikutano yote ya mtemi wa eneo hilo. Sasa kila mpiga mbinja alipoalika mikutano ya wananzengo alikuwa anawataarifu watu wakutane "HINYANGA". Kwa mfano anasema kwa Kisukuma "Ilibanza liswe ligubiza Hinyanga" yaani mkutano wetu uyafanyikia chini ya mti Inyanga. Sasa Wazungu wakashindwa kutamka "HINYANGA" badala yake wakawa wanasema "SHINYANGA"
 
Mnatuvuruga ipi asili ya hilo eneo sasa, mmeleta story 3 hebu jadilianeni kwanza!..
 
Wasukuma na wanyamwezi jadilini mje mnatuchanganya na makinikia ya jina la Sinyanga
 
Back
Top Bottom