Asili ya neno "Afrika"

Asili ya neno "Afrika"

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Historia ya dunia inasema kuwa binadamu wa kwanza aliishi barani Afrika na mifupa yake iligundulika Afrika tena katika nchi ya TANZANIA

.Na dunia nzima inajua kuwa mtu wa kwanza aliishi hapa Tanzania.wakati huo huo historia inadai kuwa sehemu ya kwanza kwa binadamu kustaharabika na kuendelea kisayansi ulianzia hapa hapa Afrika tena huko Afrika kaskazini katika nchi ya Misri.

Hivyo basi mwisho wa siku utakuja kugundua kuwa bara la Afrika lina historia ndefu sana. Lakini wewe kama mwafrika unapaswa ujue kuwa, Kuna tofauti kubwa kati ya maneno haya, Mwafrika, Uafrika na bara la Afrika. Wakati tukifikiria tofauti ya maneno haya, hebu tuone asili ya neno Afrika. Lakini kabla ya kuapata historia ya neno Afrika, kuna mambo machache ya kufahamu.

Twende kazi sasa
Kwanza Afrika ni bara la pili kwa ukubwa wa kilomita za mraba 30,221,532, lenye idadi ya watu zaidi ya 3.1 bilioni. kwa sasa bara hili lina nchi zisizopungua 56.

Kijiografia bara hili limezungukwa na bahari kubwa, kwa mfano bahari ya Hindi na Atlantiki. Na bara hili linagawika ktika sehemu kuu nne yaani Afrika kaskazini, Afrika mashariki, Afrika kusini na Afrika magharibi.

Historia ya neno Afrika inaongozwa na nadharia mbalimbali moja wapo ni nadharia ya Kabila la Waafr(Afri tribe). WaAfri ni kabila ambalo lilikuwepo kwa miaka mingi huko Afrika kaskazini. Na historia inasema kuwa waafrika hao walikuwa na vita na watu wa ulaya muda mrefu sana kuanzia miaka ya 400-100KK au KM. Na moja ya kubwa ilikuwa vita vya Punic(260-140)KK au KM ambavyo vilihusisha mapigano kati ya wacarthege(watunisia kwa sasa) na waroma.Waroma walipofika katika mji wa carthage walikuta watu( kabila la Waafri ambao kwa wakatii huo hawakujulikana waliitwaje kwa sababu za kukosekana kwa maandishi). inasemekana kuwa sababu za Waroma kuwaita Waafri ni namna ya Uongeaji wao na muonekano wao hasa hasa rangi.

Historia inaeleza zaidi kuwa, waroma kwa Lugha yao walitamka AFRICUS, wakimaanisha (the land of afri) yaani Ardhi ya waafri. na kwa kuwa hiyo ndiyo sehemu yao ya kwanza kufika, na ndio sehemu za mwanzo miji kuendelea. wakaandika habari zote juu ya Waafri na ardhi yao(yaani bara la Afrika). Kuanzia hapo maeneo hayo yalifaamika kama Africus. Na kutokana na miingiliano ya watu mbalimbali , watu wengi (hasa hasa Waarabu) walishindwa kutamka Africus na kujikuta wakitamka Afrika. Na hapo ndipo asili la neno Afrika lilitokea. jambo la kusisitiza ni kwamba, hii ni nadharia tu ambayo ilianzishwa kwa lengo la kutoa ufafanuzi. na kuna nadharia zingine pia. na zaidi waafrika tunapaswa kufahamu kuwa, asili ya mambo mengi duniani imetokana aidha mitazamo ya wageni kwa utani au mambo yao au mitazamo ya wenyeji na mtindo wao wa maisha.

Ni mimi MJUKUU WA CHIFU a.k.a kiboko ya The bold
 
Ukiangalia historia vizuri hata Adam hakuwa binadamu!
kwanini?!

Sisi ndio binadamu sababu tumefuata ubini kutoka kwa adam!d'u understand wht am talkn abou?!Adam hakuwa binadam sijui alikuwa nani?
 
Na we km mkali kuliko ze bold!embu tuletee jina ulaya limetokana na nini?!maana mi najua kuna viaz ulaya,kuku ulaya,mbuzi ulaya sijui na jembe Ulaya.
 
ukiangalia historia vizuri hata Adam hakuwa binadam!
kwanini?!
sisi ndio binadamu sababu tumefuata ubini kutoka kwa adam!d'u understand wht am talkn abou?!Adam hakuwa binadam sijui alikuwa nani?
labda alikuwa Jini[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Nilisikia africa ilitokana na mtindo wa kubeba wafalme wetu na ma chifu kuwaweka began wazungu wakasema the land of "A FREE CAR" so baadad watu wakaunganishs kuwa AFRICA
 
Ukiangalia kwa makini Biblia inasema binadamu wa kwanza ni Adam, fuvu lake lilipatikanaje Afrika tena Tz??? Nikiamini historia basi napingana na dini? Contradiction!! What's the truth? Naweka kakiingereza kwa msisitizo
 
Nimeona umezungumzia afrika imegawanyika ktk pande nne, ukataja north africa,south africa,west africa na east africa. Vip africa hatuna central africa?
 
Ukiangalia kwa makini Biblia inasema binadamu wa kwanza ni Adam, fuvu lake lilipatikanaje Afrika tena Tz??? Nikiamini historia basi napingana na dini? Contradiction!! What's the truth? Naweka kakiingereza kwa msisitizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Biblia ni historia iliyoandikwa miaka mingi kabla ya KK. Fuvu kupatikana Tz ni 1959. Hii imetokana na uchunguzi wa kisayansi.

Maswali ya tathmini
1. Historia iliyoandikwa miaka mingi inaweza kuwa ni hadithi za kutunga?

2. Science kwa kutumia njia za kisayansi kama carbon 14 inaweza ikafanya makosa?

3. Kwa kuwa ukusanyaji taarifa za kisayansi hazikupi jibu la moja kwa moja isipokuwa lazima utafsiri. Je tafsiri ya wanasayansi inaweza kupotosha.

4. Kwa kuwa katika kutafsiri maoni ya mtu yana nafasi kubwa, yawezekana maoni ya wanasayansi hao yakawa hayataki kusikia habari za dini makusudi?
 
Nashukuru kwa maoni yako mazuri, historia ni kitu kilichokuwepo eg historia ya Mkwawa ni mtu kweli aliyeishi miaka hivyo. Lakini hadithi inatungwa tu, samahani sipotoshi ila Adam ni hadithi tu hapakuwepo na mtu huyo. Basi wanasayansi waliona fuvu wakafanya tathmini ya kisayansi, labda waseme fuvu la kale zaidi lakini sio mtu wa kwanza. Mtu wa kwanza labda ufunuo wa Muumba hakuna binadamu anaejua. Hata wanasayansi wanasema kitu kinachokaribia ukweli anaejua ukweli ni Muumba
 
Back
Top Bottom