Asili ya siku ya wapendanao (Valentine’s day). Haipo kama ambayo sisi tunaichukulia

Asili ya siku ya wapendanao (Valentine’s day). Haipo kama ambayo sisi tunaichukulia

Street brain

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2022
Posts
584
Reaction score
767
Siku ya Valentines Day asili yake ni kutoka Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memoria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi

Sababu ya kutetea waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu. Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya ulimwengu kuisherehekea kama siku yamapenzi kinyume cha dhamira ya Mt. Valentine.

Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za kueneza dola ya kirumi duniani kote na hivyo vijana hawakutakiwa kuoa, ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi.

Wakioa hawangekuwa na uhuru wa kwenda vitani bali kuwa na famiia zao. Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada tu kitu ambacho kanisa lilikukwa linapinga.

Padre Valentine ambaye alikuwa Roma akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele ya Mungu.

Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi.

Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kuuawa kama shahidi mfia dini kwa ajili ya kutetea waamini wake wafunge ndoa badala ya maisha ya ngono zembe bila ndoa.

Wakristo wakawa siku ya kumkumbuka Padre Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kuwa wanandoa. Ikaenea katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka Mt. Padre Valentin.
By Clement
 
Haijalishi chimbuko ni wapi kikubwa imeshapitishwa kua siku ya Wapendanao na iwe hivyo, kwanza sijaona tofauti kama Valentine alitaka waliopendana wafunge ndoa sio ndio maana ya upendo huo.

Tukianza kuchimbua chimbuko la maadhimisho tutajikuta na siku ya Uhuru tu mengine yatakua batili.

Upendo sio lazima uwe na mpenzi tunahimizwa sasa hivi kujipenda wenyewe.
 
Upendo unapowekewa siku maalumu ni ubatili tu...

Watu wanapaswa kupendana siku zote, majira yote, hali yoyote...
 
Valentine's day

 
Back
Top Bottom