Asili ya Vita vya mashariki ya Congo.

Asili ya Vita vya mashariki ya Congo.

mike2k

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
1,571
Reaction score
3,448
CHIMBUKO KUU LA VITA NA MAPIGANO NCHINI CONGO DRC.

Ni muhimu sana kuelewa historia kujua kwanini hadi sasa kuna vita hizi na mapigano haya. Ndani ya nchi ya Congo DRC kuna makabila mengi ikiwa ni pamoja na kabila la 'Banyarwanda ' au Banyamulenge (Watu wa Mulenge) Mulenge ni eneo ndani ya Kivu ya Kusini ambao ni wakongomani ila wenye asili ya Rwanda na wanaongea Kirwanda (Rwandaphones) ambao wapo Congo ya Masharìki (Eastern Congo ) yaani Kivu ya Kusini na Kaskazini. Ambapo ni mpakani mwa Rwanda na Congo na wapo 5% ya idadi ya watu wote ndani ya Kongo.

View: https://x.com/OlengurumwaO/status/1885713447507177687?t=fPDbbEUI2-bgF4KWTyZOeg&s=19
Swali Je, hao Banyarwanda au Banyamulenge au Congolese Tutsi ilikuwaje ni Wakongomani wanaongea Kinyarwanda?.

Kabla ya Wakoloni kugawa mipaka ya Rwanda,Burundi na Congo Free State . Kulikuwa na falme wa Kingdom of Rwanda chini ya Mwami ambayo ufalme\himaya hii ilikuwa hadi maeneo ya Kivu eneo ambalo sasa lipo ndani ya Congo. Wakati wa kugawa mipaka katika Mkutano wa Berlin 1884-1885 ndipo kukapatikana Congo Free State chini ya Beligiji (Belgium King Leopard II) na Rwanda na Burundi kubaki chini ya Mjerumani . Baada ya mipaka hii kuna watu ambao walikuwa sehemu ya Rwanda wakajikuta wapo eneo la Congo Free State chini ya himaya ya Beligiji King Leopard II ambapo ni mpakani mwa Rwanda (Congo ya Masharìki)Kivu ya Kusini na Kaskazini.

Sababu ya pili, baada ya vita ya kwanza ya Dunia 1914-1918 Makoloni yote ya Mjerumani yalikuwa chini ya uangalizi wa League of Nation baada ya Mkutano wa Verssaile Peace Treaty. Hivyo Makoloni ya Burundi na Rwanda ambayo yalikuwa chini ya Mjerumani yakawa chini ya Mbeligiji King Leopald kuyasimamia kwa uangalizi wa League of Nation. Hivyo sababu Burundi ,Rwanda na Kongo zote zilikuwa chini ya Belgium hivyo muingiliano ukazidi kuwa mkubwa sana kwani Beligiji alikuwa anachukua watu kutoka Rwanda kwenda kwenye mashamba ya Masharìki ya Congo ,Kivu ya Kaskazini hasa miaka ya 1950. Hivyo uwepo wa Wanyarwanda wakitusi ukawa mkubwa katika maeneo hayo kutokana na muingiliano.

Miaka yote uwepo wa Watusi wakikongomani wanaongea Kinyarwanda haijawahi kuwa tatizo katika Kongo ya mashariki. Na sheria mbalimbali zilitungwa kuwatambua mfano sheria ya uraia ya 1971 na 1981.Wote ambao ancestors wao na wao walikuwepo nchini Congo tangu kugawiwa mipaka na wakoloni hadi Congo/Zaire ilipopata uhuru 1960 ni Raia wa Congo.

Ni sawa na kabila la wajaluo wa ambao wapo Magharibi mwa Kenya ,Masharìki mwa Tanzania na Kaskazini mwa Uganda ambao walitenganishwa na mipaka iliyowekwa na wakoloni ,huwezi kusema Wajaluo wa Tanzania ni Wakenya sio watanzania.

View: https://x.com/Labella_Mafia95/status/1884916819590283408?t=fPDbbEUI2-bgF4KWTyZOeg&s=19
Ni sawa na Wamanyema (Wagoma,Wabwari,Waholoholo) wa Mkoani Kigoma.Huwezi sema wamanyema wa Tanzania Kigoma ni wakongo sio Watanzania, Ni sawa na Waha wa Tanzania huko Kigoma ambao lugha yao inafanana na Kirundi na Kinyarwanda huwezi kusema Waha wa Tanzania ni warwanda au Warundi, ni sawa na Wamasai wa Tanzania na Kenya huwezi kusema Wamasai wa Tanzania ni Raia wa Kenya, hata huko Congo ya Masharìki (Kivu ya Kusini) maeneo ya Katanga na Lubumbashi kuna Wakongomani wanaongea Kiswahili huwezi kusema hao sio wakongo ni wa Tanzania.

Changamoto ilianzia baada ya Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda 1994 , baada ya wahutu kuamua kuuwa na kuchinja watusi ,ongezeko kubwa la Watusi wakakimbilia Masharìki ya Kongo (Kivu).

Elewa hapa ,kuna watusi waliokuwepo Kongo miaka na Miaka ,maeneo ya Masharìki ya Kongo (Kivu kusini na Kaskazini) mpakani mwa Burundi na Rwanda ambao walikuwepo miaka na miaka na waliotokana na kugawiwa kwa mipaka ya wakoloni,waliosafirishwa kutoka Rwanda kama wafanyakazi wa Kikoloni mashambani ambao wote hawa walitambuliwa kama Raia katika sheria ya 1971 na 1981 . Na kuna watusi ambao walikimbilia Congo kama wakimbizi kutokea Rwanda miaka ya 1994 wakati wa mauaji ya Kimbari .

View: https://x.com/OlengurumwaO/status/1885672853237801225?t=GfR_nOGxgXbPSH8JbPxAZg&s=19
Hivyo Congo ikawa na watusi aina 3 ,waliokumbwa na mipaka ya wakoloni wakajikuta ni watusi waliopo Congo, watusi waliochukuliwa na Beligium kama wafanyakazi kwenye mashamba kutoka Rwanda kwenda Congo na Watusi waliokimbia kama wakimbizi wakati wa mauaji ya Kimbari na wengine walikimbia vita Burundi wote hawa wapo Congo ya Masharìki (Kivu Kusini na Kaskazini).

Mapema tarehe 28/April/1995 Serikali ya Zaire (Congo ) chini Mobutu Seseko na Bunge lake wakapitisha azimio la Uraia ya kwamba Banyarwanda wote (Raia wa Congo wenye asili ya Rwanda) ni wageni (Foreigners) na walio bahatika kupata uraia wa Zaire /Congo walipata kwa udanganyifu (Fraudulently).

Na October 31,1996 Bunge la Zaire likatangaza kuwafukuza watu wote wenye asili ya Rwanda ,Uganda na Burundi ambao wengi ni watusi wenye asili ya Rwanda.

Hii ikapelekea kuibuka kwa makundi ya waasi ndani ya Masharìki ya Congo.(Kivu kusini na Kaskazini) dhidi ya Serikali ya Congo. Na hapa ndipo Rais Kagame akapata tobo la kupitia , tuelewe ya kwamba katika mauaji ya Kimbari nchini Rwanda. Wahutu ambao ndio walikuwa wengi 85% ya idadi ya watu walianza mauaji dhidi ya watusi baada ya Rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana ambaye alikuwa mhutu kuuwawa April 1994 kwa ajali ya ndege.Wahutu wakadai ni waasi wa RPF chini ya Kagame ndio wamedungua ndege. Hivyo wahutu wakaanza kuwaua watusi.

Lakini baadaye Jeshi la waasi chini ya Kagame liitwalo RPF - Rwandan Patriotic Front likafanikiwa kukamata nchi ya Rwanda ,na wauaji wengi wa kihutu (Genociders) walikimbilia nchi ya Zaire na kupewa hifadhi na Mobutu Seseko. Na baadaye wakaunda kikundi cha waasi dhidi ya Rwanda na wanajeshi wa Rwanda kikundi hicho kikaitwa FDLR (Democratic Forces for the Liberation of Rwanda ) ambacho hadi sasa bado kipo. Hiki ni kikundi cha waasi ndani ya Kongo kinachotokana na wahutu waliokuwa wanajeshi wa Rwanda kabla ya mauaji ya Kimbari (Ex-Rwandan Armed Forces )(Interahamwe) au Genociders wakakimbilia Kongo na kujificha huko Congo ya Masharìki ambao wapo kinyume na Watusi na Serikali ya Rwanda pia.

Kikundi hiki ndio tishio kwa Kagame . Sasa Kagame akaamua kuunga Mkono vikundi vya waasi wa kitusi vilivyopo Kongo ya Masharìki dhidi ya Serikali ya Mobutu Seseko , na kuunga mkono kikundi cha waasi cha Alliance of Democratic Forces for Liberation of Congo chini ya Laurent Kabila 1996 dhidi ya Mobutu Seseko .

Hata alipoingia Laurent Kabila ,baadaye Joseph Kabila na hata Felix Tshisekedi kosa kubwa wameendelea kulifanya ni kuendelea kuwakumbatia waasi wa FDLR ambao ni wahutu (Genociders) Interahamwe. Na sababu Jeshi la Congo ni dhaifu FDLR wamekuwa wakitumiwa na Serikali ya Kongo dhidi ya waasi . Hili ndio linapingwa na Kagame sababu Kagame anaona hao FDLR kuendelea kuwepo na kuwezeshwa ni tishio kwa Kagame wanaweza rudi kumg'oa hivyo ndio maana na yeye amekuwa akisaidia M23 na Jeshi la Rwanda (Rwandan Army Forces ) limekuwa likishirikiana na waasi na kutoa support dhidi ya Serikali ya Congo ,Jeshi la Congo FARDC na FDLR.

SULUHU YA MGOGORO HUU.

1.Kundi la waasi la FDLR (Democratic Forces for the Liberation of Rwanda ) ambalo ni kundi la waasi la kihutu wanaofahamika kama INTERAHAMWE (Genociders) waliokimbilia Kongo lisambaratishwe(Disarmed) ili Kagame akose sababu ya ku support M23. Na hii inaweza saidia kupunguza tension ya vita na mapigano Masharìki ya Congo. Kuliwahi kuwa na azimio la SADC Summit, UN,ICGLR kutaka FDLR kujisalimisha na kusalimisha silaha na kuvunja kundi. Na FDLR walikuwa tayari 2014 ila sijui kwanini hakukuwa na utekelezaji.

2.Kagame akome kujihusisha na masuala ya Kongo DRC. Jumuiya ya Afrika (AU),EAC ,SADC na UN wote kwa pamoja wampe onyo RWANDA na Uganda kuacha kuingilia masuala ya Kongo ,waache kutoa misaada ,waache kuingiza majeshi yao nchini Congo.

3.Serikali ya Congo iwaone Wakongo wote wenye asili ya Rwanda (Congolese Tutsi) au Banyarwanda /Banyamulenge iwaone kama Raia wakongo na wanaopaswa kutendewa na kupewa haki sawa kama Raia wa Congo ,wasichukuliwe kama ni Wanyarwanda eti sababu wanaongea kinyarwanda . Waajiriwe katika vyombo mbalimbali kama Raia wengine . Serikali ya Congo iache Ubaguzi ,ielewe ya kwamba Banyarwanda au Banyamulenge sio Raia wa Rwanda ni wa kongomani. Ifanye mazungumzo na M23 kama watusi wa Congo na isiwaone kama Watusi wa Kirwanda.

Na hii itasaidia kumfanya Kagame kupoteza sababu ya ku sympathy kinafiki na watusi walioko Masharìki ya Congo ambao ndio hao M23 ili kujinufaisha. Kagame amekuwa akitumia watusi wa Masharìki ya Congo kwa manufaa yake huku akijifanya kuwaonea huruma ,pia Kikundi cha FDLR kuwepo Congo imekuwa ni kisingizio kikubwa cha Kagame kuendelea kuchochea vita na mapigano Kongo kwa faida yake binafsi ,pia hata waasi wa M23 wamekuwa wakitumia sababu ya kutengwa na kubaguliwa kama kigezo cha wao kuendelea kupigana ikiwa wana maslahi binafsi juu ya Rasilimali za Congo ,na hizo sababu za kubaguliwa na kuonewa ndio wamekuwa wakizitoa kwa umma ili kupata kuungwa mkono kwamba wao ni watetezi wa watusi ndani ya Masharìki ya Congo . Hivyo kutekelezwa kwa hayo mapendekezo matatu hapo juu yatasaidia kuonesha dhamira ya kila kundi na kila mmoja katika Mgogoro huu,ieleweke Mgogoro wa Congo umekuwa na wanufaikaji wengi sana kwa Rasilimali zilizopo Congo. Na ndio sababu ya Mgogoro huu kuendelea kuwa mkubwa.

Abdul Nondo. (FACEBOOK)
 
Nimeelewa vizuri sana mike2k
 
Back
Top Bottom