Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,483
- 2,392
Kuna Mfanyabiashara mburushi wa Mbalali alikutwa na Meno ya Tembo na Bunduki zaidi ya 10 ni ndugu na ROSTAM Kesi iliishi kisutu kwa kupigwa faini Mil 20Kama hujagundua hili bado wewe hufikirii sawasawa. Watu wote hupenda kuwa CCM na kupigania kupata nafasi zaidi na zaidi kama sehemu salama ya kujifichia maovu na haramu.
Hii inahusu viongozi wote kuanzia juu mpaka chini. Kuanzia mwenyekiti wa shina mpaka namba moja. Chunguza hilo bila kutumia nguvu utagundua.
Mfano mdogo tu ni hili sakata la uhamiaji na gari lililodakwa likivusha wahamiaji haramu 20. Gari hilo linatajwa kuwa mali ya Habib Nasser. Huyu ni mwenyekiti wa CCM kata ya Ilala na mjumbe wa Baraza Kuu Jumuiya ya Wazazi CCM-DSM.
Hiyo bendera ya CCM haikuwekwa bahati mbaya, alijua uhakika. Hiyo ni ajali kazini au kuna watu walimchoma. Tofauti na hapo, goma likishakuwa na bendera ya chama trafiki wanapunga mkono tu unateleza.
Hawa matajiri wanaopambania vyeo vya udiwani, ubunge lengo namba moja inakuwa kuficha vitu vyao haramu ikiwemo ukwepaji kodi. Hivyo hivyo kwa watu wa kawaida. Lengo namba 5 ndio inaweza kuwa kutumikia nchi.
Hata hawa vijana unaowaona humu mitandaoni ikiwemo JF ni njaa tu hakuna kingine.
Watch out mzee baba