Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Asilimia 4 ya Watanzania wana matatizo ya macho huku zaidi ya asilimia 90 ya matatizo hayo ya macho yanatibika.
Amesema Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassm Majaliwa kuzindua jengo la Idara ya Macho lililojengwa kwa thamani ya Shilingi Bilioni 3.7.
“Umekuja kuzindua jengo hili ambapo kwa ukanda huu watu hawatokwenda tena KCMC Kilimanjaro au Dar Es Salaam kufuata huduma za macho,” amesema Dkt. Mollel.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua Jengo la Huduma za Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ambalo limejengwa kwa thamani ya Shilingi Bilioni 3.7 ikijumuisha na uwekaji wa vifaa tiba kwa ajili ya huduma za matibabu ya macho.
Upanuzi wa huduma za matibabu ya macho katika Kanda ya Ziwa kutawapunguzia adha wananchi kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma hiyo ambayo awali walikuwa wakisafiri kwenda Kilimanjaro, Dodoma au Dar es Salaam kupata huduma hiyo.
=========
Oktoba 2021 akiwa Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima alisema takwimu za Tanzania ni watu milioni 1.2 tu kwa mwaka 2020 ndio waliofikiwa na huduma za macho katika vituo vya kutolea huduma za afya ikilinganishwa na uhitaji wa takribani watu milioni 12.