Asilimia 40 ya magoli waliyofungwa Madrid La Liga yamepitia kwa Marcelo.

DesertStorm

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2015
Posts
3,131
Reaction score
2,537

Asilimia 40 ya magoli waliyofungwa Madrid La Liga yamepitia kwa Marcelo.

Real Madrid wana tatizo kubwa upande wa ulinzi wa kushoto ambapo ni jukumu la beki wa kibrazili Marcelo.
Magoli ya Celta Vigo katika mchezo wa wikiendi iliyopita yote yalitokana na udhaifu wake upande wa kushoto anapopanda kushambulia na kushindwa kurudi nyuma kwa uharaka na kuzuia hatari zinazoelekezwa langoni.
Msimu huu pekee kwenye La Liga. Real Madrid wameruhusu magoli 16, magoli 6 sawa na asilimia 40 ya magoli hayo, yalipitia upande wa Marcelo.

Kwa jinsi navyoona huyu babu Mzimu wa Messi bado unamuandama sana,, ile siku ya El Clasico ilikuwa sio shughuli ndogo kumkaba Messi,, walitepeta mno mpaka wakampumzisha Casemiro,, yani ilibakia kidogo sana wavunjwe kiuno yeye Ramos na Casemiro wao. Messi sio wa dunia hii.

Karibuni wadau!!!!
 

6/16 x 100=37.5%. Hiyo 40% umeitoa wapi?



https://www.whoscored.com/Players/20241/Show/Marcelo
 
huyu hata mie namhusudu sana ana bidii sana uwanjani
 
Ndo maana mtoto wangu wa pili baada ya swalehe ntamwita Marcelo !!! Et mama ake alitaka nmwite chirwa hahaha daah [emoji23] [emoji41] huyu jamaa namkubali sijali watakachosema anajua mpira na mpira unamjua nkikumbuka mechi ya juve !!!
 
Ndo maana mtoto wangu wa pili baada ya swalehe ntamwita Marcelo !!! Et mama ake alitaka nmwite chirwa hahaha daah [emoji23] [emoji41] huyu jamaa namkubali sijali watakachosema anajua mpira na mpura unamjua nkikumbuka mechi ya juve !!!
Mpura - mpira
 
Yani wachezaji wa kibrazili wakishafikisha miaka 30 tu wanaanza kuwa wazito/kubweteka na matako makubwa kama mabamedi hawa jamaa sijui wana matatizo gani.sio kama mahasimu wao Argentina players
 
Ila huyu jamaa anawasaidia sana RM kwenye kuattack. Akisema abaki kwenye ulinzi sana timu itakuwa haipati magoli. Pia wat uwanamlaumu sana Kroos kutosaidia kwenye ulinzi.
 
hater wa real madrid utawajua tu kwani gerald pique ana asilimia ngapi magoli ya kufungwa barca kupita kwake
 
Jibu rahisi tu Marcello ni best right flank attackers than defence
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…