DesertStorm
JF-Expert Member
- Nov 22, 2015
- 3,131
- 2,537
Asilimia 40 ya magoli waliyofungwa Madrid La Liga yamepitia kwa Marcelo.
Real Madrid wana tatizo kubwa upande wa ulinzi wa kushoto ambapo ni jukumu la beki wa kibrazili Marcelo.
Magoli ya Celta Vigo katika mchezo wa wikiendi iliyopita yote yalitokana na udhaifu wake upande wa kushoto anapopanda kushambulia na kushindwa kurudi nyuma kwa uharaka na kuzuia hatari zinazoelekezwa langoni.
Msimu huu pekee kwenye La Liga. Real Madrid wameruhusu magoli 16, magoli 6 sawa na asilimia 40 ya magoli hayo, yalipitia upande wa Marcelo.
Kwa jinsi navyoona huyu babu Mzimu wa Messi bado unamuandama sana,, ile siku ya El Clasico ilikuwa sio shughuli ndogo kumkaba Messi,, walitepeta mno mpaka wakampumzisha Casemiro,, yani ilibakia kidogo sana wavunjwe kiuno yeye Ramos na Casemiro wao. Messi sio wa dunia hii.
Karibuni wadau!!!!