Asilimia 50 ya ndoa zote huvunjika kwa jambo hili...

GoLC

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2025
Posts
268
Reaction score
466
Wakati fulani nimekuwa nikimtizama Joel Nanauka kwa upande hasi kwenye content zake ila sasa namuelewa. Joel kama umemsikiliza vizuri au kumsoma, hoja zake nyingi ni upande wa jamii inavyochukuliana, au vile mtu mmoja anavyomchukulia mwingine. Nyuma yake pakijaa chuki, uzandiki, roho mbaya, wivu mbaya, nk.

Tukija kwenye ndoa utaona kuwa wanandoa huanza vyema sana. Tukishikilia mengine ( ceteris paribus), utaona kuwa kuna watu wake kwa waume hufanya jitihada za wazikuvunja ndoa za wengine. Ni jitihada za makusudi.

Utakuta mwanamke aliye rafiki wa mke, tena kwa kujua huanza kumweleza mkeo masuala ambayo yataleta uchonganishi.
Mfano atamwambia, wewe jipambanie.

Wanaume hawajali. Utakuta mwenzio ana mwanamke nje huko. Au ukiugua au kufariki anaoa mara moja. Wanaume sio wa kuwawekea maanani. Jinali wewe kwanza.

Maneno kama haya na mengine yakimmuta kichwa maji huyachukua na kuyafanyia kazi. Vivyo hivyo kwa wanaume, japo kwa uchache.

Ni muhimu sana mawasiliano kwa wanandoa kuwepo ili kupata fursa ya kuongea mambo menginikiwa ni pamoja na umbea. Katika huo umbea ndio mke atafunguka kukueleza ya ndani kama hayo.

Ukiwa gumegume sana hatapata nafasi ya kukupenyezea masuala ambayo unaweza kuyaona ya kijinga ila kiuhalisia yanaweza kuwa ni tiba kwa ndoa yenu. Ni rahisi kuwajua kuwajua na kukabiliana nao wafitini. Ukimjua adui ni nusu ya kushinda vita.

Sasa eneo hili la fitina wanandoa wanaweza kulipuuzia, hasa wanaume, akiamini kuwa sio levo zake kujadili petty issues na mke. Yeye atafute pesa, amfurahishe mke BASI! Kumbe mke naye keshalishwa sumu na jirani au rafiki na anakusubiria uive ive kidogo akuvune kisha aendelee kula maisha maana alishaambiwa JIJALI.

Wanandoa, hasa wanawake... Za kuambiwa changanya na zako
 
Makundi hasa mkeo akiwa urafiki na wanawake waliovunja ndoa zao kwa jina maarufu la makurumbembe yalielezewa kwa undani sana na mkuu Natafuta Ajira

Makundi haya yakiambatana na wanawake walivunja ndoa kisha wakaolewa tena hurudi kwenye ndoa ya2 kwa Timing vibaya mno kwani yana amini yataendwa tena.

Hawa makurumbembe ndo mabanigwa wa kuwashauri wanawake wenye ndoa changa kama ulivyoelezea hapo.

Ni wajibu wa kila mwanaume kupinga kwa namna yoyote Ile mke wake akiwa na ukaribu na haya makurumbembe daima hayana jema kwenye ndoa za wengine.

Yanapigo zote haya umala,ulevi na anasa zote hayana mipaka.
 
Kweli kabisa. Tatizo wengine ni ndoa zao za kwanza tatizo wana asili ya ufitini
 
Naimiss sana jf ya enzi zile kipindi mada zilikiwa zinachambuliwa kwa hoja haswa. Leo hii ni majanga
 
Pole mkuu ume comment kwa idea mpya joined 2025,

Anyway wengi tuiopo humu ni vijana saizi ya kati kwa sasa wale wazee wengi wameshajifia,pengine zoea hilo.
Wengi wetu hatujaoa ndui maana unaona wengi wanakataa ndoa

Ni vipi ukatoa maoni kuhusu ndoa ingali hujaonja tamu na chungu ya ndoa

Wazee wetu wamebaki kina Bufa labda.
 
Tumeacha vijana mshike hatamu. Sisi tunaangalia tu.
 
Pole mkuu ume comment kwa idea mpya joined 2025,

Anyway wengi tuiopo humu ni vijana saizi ya kati kwa sasa wale wazee wengi wameshajifia,pengine zoea hilo.
Wengi wetu hatujaoa ndui maana unaona wengi wanakataa ndoa

Ni vipi ukatoa maoni kuhusu ndoa ingali hujaonja tamu na chungu ya ndoa

Wazee wetu wamebaki kina Bufa labda.
Sio suala la kujisifia wala kufurahia kuwa na mtizamo huo. Ukifikia levo uliyofika ni rahisi sana kuwa na woke mind. WOKE sio WAKE au WORK. WOKE
 
Una maana gani mkuu sikuelewi mbona
 
Back
Top Bottom