Elections 2010 Asilimia 50 ya wanaomaliza STD VII hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu!

Elections 2010 Asilimia 50 ya wanaomaliza STD VII hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu!

Labda wangetusaidia kutueleza waliofanya utafiti walitumia population za shule za aina gani? hii ingeleta maana zaidi, ni kweli 50% hawajui kusoma lakini kwa picha kubwa zaidi tunahitaji kujua wanatoka kwenye shule za Accademia au kazana twende?

Wakitoa population waliyotumia kufanya utafiti inawezekana wametumia kazana twende peke yake hii itakuwa na maana nyingine kubwa ambayo watu wanaiopigia kelele ambayo ni tatizo la ujenzi wa matabaka kwenye elimu kwa kutengeneza watawala na watwana wa baadae

Hawa wanaosoma kwenye kazana twende watakuwa wavuta bangi, wezi na majambazi. Baadae tutawalaumu na kuwachoma moto au kuwapeleka mahakamani ili wahukumiwe na hakimu aliyesoma academia.

Government need to think twice kwenye mfumo wa elimu tunaoenda nao kwa sasa

Obviously ni Shule za Msingi za Serikali
 
this is also kikwete`s fault ???!! kama mtoto ni kiazi .. ni kiazi tu!! miaka 7 mwalimu anakuja darasani kukufundisha alafu usijue kusoma wala kuandika!
 
this is also kikwete`s fault ???!! kama mtoto ni kiazi .. ni kiazi tu!! miaka 7 mwalimu anakuja darasani kukufundisha alafu usijue kusoma wala kuandika!
lol..
Kiazi nadhani ni wewe ambaye hujui hata unachoongea..hizo shule zinazotoa wahitimu wasiojua kusoma na kuandika una uhakika zina walimu au walau wa kutosha? vitabu + stationaries je? madarasa yenye kukalika, madawati?? hello? r u there?
 
Hii habari nayo iwe sehemu ya kampeni ya mgombea wa CCM maana wanavuna wanayopanda. Badala ya kulisogeza Taifa mbele, wananchi wengi wanarudishwa nyuma. Ni familia zao tu na wale wanaowaweka madarakani ndio wanaonekana kupeta.
 
Tanzania kuna sheria yoyote inayohusiana na home schooling?
 
this is also kikwete`s fault ???!! kama mtoto ni kiazi .. ni kiazi tu!! miaka 7 mwalimu anakuja darasani kukufundisha alafu usijue kusoma wala kuandika!

Wewe na Kiranga mnafikiria sawa kabisa... Kiranga atakuambia kuwa haya yote ni makosa ya ujamaa na Nyerere. Ingekuwa shule zote ni za kulipia (ooppssss nimesahau kwa shule zinalipiwa majengo, madawati na michango kibao isiyokwisha) haya yote ..... hata nimesahau point yake huwa ni ipi hasa
 
this is also kikwete`s fault ???!! kama mtoto ni kiazi .. ni kiazi tu!! miaka 7 mwalimu anakuja darasani kukufundisha alafu usijue kusoma wala kuandika!
Yes, this is JK's fault. Kama hili sio tatizo la JK ni tatizo la nani? Viongozi tunawapa majukumu kwa malengo gani??Nani kakudanya kuwa watoto wote hao ni viazi. Inawezekana wewe ndio kiazi bila kufahamu ni kiazi kwa kuwa una neemeka na uwepo wa JK madarakani.
Kama wanafunzi hawana walimu, vitabu vya kujisomea na mazingira mabovu ya kujifunza unategemea matokeo yatakuwaje?
Mbona JK anaona sifa kuongeza idadi ya shule za sekondari bila kuzungumzia lolote kwenye madawati, walimu, maabara na miundo mbinu mingine ya elimu??
Tusiifanye ikulu na uongozi wa nchi ni sehemu ya kujineemesha wachache tukasahau kuwa pale ndipo mzogo wote wa maendeleo na ustawi wa nchi yetu ulipo. Kwa bahati mbaya kuna watu tunapiga kampeni kwasababu tunaneemeka na watu wasiotaka kuchukua responsibility zao kuona Taifa linasogea mbele.
Haya ndio mambo ambayo CCM ikiendelea kuyafanyia mchezo, itajikuta inaingia kaburini siku sio zake. Wananchi wana nguvu kuliko system yoyote hapa ulimwenguni. Tusiendelee kuwadharau kama vile hawaoni wala hawana uwezo wa kuamua hatima ya Taifa lao. Tutalia wenyewe siku moja.
 
Elimu ya leo ni ngumu kwa kweli.
My wife wangu ni mwalimu shule ya msingi - kuna wakati alikuwa anafundisha darasa lenye watoto karibu 200 katika chumba kimoja darasa. Licha ya watoto kutokuelewa pia shule zinakuwa janga la kiafya!
 
Kulaumu pasipo kufahamu sababu ni sawa na kwenmda kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya Malaria. Na kibaya zaidi hawa wote wanaolaumu elimu ya bure ndio walifanya vizuri wakati wa Nyerere na leo hii ni masomi wanaoongoza nchi na wengine hata kutoa taarifa za uongo kuhusiana na elimu ya bure ambayo wao wenyewe ni kizazi cha elimu hiyo.

Quality of education haihusiani kabisa na shule kuwa bure au kulipia. Nitarudia kusema tena nchi zote zinazoongoza ktk elimu bora dunia zinatoa elimu ya bure kwa wananchi wake. Hata Nchi ndogo kama Porto Rico zinasifika leo duniani kwa mafanikio kwa sababu hawa wote wanazingatia elimu kwa WATU na MAZINGIRA yao.. Leo Tanzania kila shule ina syllabus yake regardless of the medium of instruction, tena basi wengi wana prefer kiingereza kitumike kama medium hali watoto wetu hata lugha hiyo hawaifahamu.

Ndio maana vijana wengi nchini wanaweza kuzungumza kiingereza lakini hawawezi kusoma kitabu kilichoandikwa kiingereza kwani tumeshindwa kuelewa tofauti baina ya kiingereza kama lugha na kiingereza kama elimu. Hata huko Uinngereza kwenyewe wapo waingereza wasioweza kusoma hivyo kumfundisha mtu lugha haina maana atakuja jua kusoma pia..Na hali kadhalika mtu hawezi kujua kusoma pasipo kuijua lugha kwanza..kama hajui lugha huwezi kusoma na ukaelewa maana vile vile kama hujui kusoma hutaweza kuandika au hata kufanya hesabu kwani elimu inaanza na kujua kusoma na kuandika. Lugha pekee sio ELIMU, huu ulimbukeni wa kufikiria kwamba elimu ni kiingereza pasipo kuzingatia watu na mazingira yao ni ubishi ulotufikisha ktk matunda haya. kifupi, Mbili kujumlisha na mbili haiwezi kuwa jibu tofauti na two plus two ila kuna urahisi na uwezekano mkubwa wa mtoto wa Kitanzania (darasa la kwanza) kuelewa jibu la mbili kujumlisha mbili kuliko two plus two.

Nachoweza kuchangia katika elimu yetu ni kufahamu kwamba kiingereza kinatakiwa kifundishwe kwanza kama Lugha toka darasa la kwanza ili kumwandaa mtoto apate kujijua lugha ya kufundishia akifika darasa la tano. Wakishajua lugha ndipo unaweza kuwafundisha masomo kwa lugha hiyo lakini sii kuwapachikia masomo kwa kiingereza hali hawajui hata neno moja la kiingereza. Toka darasa la kwanza kiingereza (lugha) iwekewe umuhimu zaidi ili wanafufunzi watakapo fika darasa la nne wawe tayari wameweza kui master lugha kisha ndipo unaweza wafundisha kwa kiingereza..Ni matatizo ambayo sisi Waislaam tunayapata sana katika elimu ya dini na ndiuo maana wengi ni mbumbumbu ktk elimu yadini zaidi ya
 
Back
Top Bottom