Asilimia 61 ya eneo la Tanzania hatarini kugeuka jangwa

Asilimia 61 ya eneo la Tanzania hatarini kugeuka jangwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Zaidi ya asilimia 61 ya eneo la Tanzania inakabiliwa na hatari ya kugeuka jangwa ikiwa juhudi zaidi hazitachukuliwa kukabiliana na changamoto za uharibifu wa misitu ya asili unaotokana na ongeeko la shughuli za binadamu zisizo endelevu na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Wataalam wa misitu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Timotheo Mande na George Miringay kutoka Ofisi ya RAIS TAMISEMi wameshauri juhudi zaidi ziongezwe katika uhifadhi wa misitu ya asili ili kuinusuru nchi katika hatari ya kugeuka jangwa.

Hayo yamebainishwa katika mkutano wa Wataalam wa Misitu na Mazingira wa kuandaa mkakati wa Tanzania kuhifadhi na kurejesha zaidi ya hekta milioni tano na laki mbili za uoto wa asili chini ya mkakati wa dunia wa Bonn Challenge wa kurejesha hekta milioni 350 ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (WWF) Dkt. Severin Kalonga amesema WWF Tanzania imekuwa mdau muhimu ikishirikiana na Serikali ya Tanzania kutafuta fedha kwa wadau wa kimataifa wa mazingira ili kufanikisha utekelezaji wa mkakati huo muhimu kwa uhifadhi wa misitu.
 
Zamani kule kwetu Mlimba,kidenge,Mpanga hadi masagati kulikuwa na misitu mingi sana,huko wilaya ya Kilombero,lakin tangu miaka ya 2005 wakaanza kuja na kujaa kwa wingi hawa jamii za wafugaji(Wasukuma) bhas wanakata miti hovyo kwa ajiri ya kilimo na mifugo.

Leo hii Mlimba sio ile ya miaka ya nyuma ya kuvutia kwa misitu na vichaka vizuri ni uwala tu,jangwa linatengenezwa hata wale wanyama jamii ya Simba na Chui walishatoweka
 
Watu wameimaliza miti ya mikalambati yote. Mivule unaitafuta kwa tochi.
 
Back
Top Bottom