John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Madaktari Bingwa 30 hutoa huduma katika Hospitali ya Rufaa Amana Wilayani Ilala.
Hayo yalisemwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Amana, Dkt.Bryson Kiwelu katika madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo alishiriki siku hiyo na Watumishi wake Wanawake.
Dkt.Bryson Kiwelu alisema wanawake ni nguzo muhimu katika familia piani watendaji katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
"Katika hospitali yetu ya Rufaa Mkoa Amana asilimia 70 Wauguzi wetu wanaotoa huduma wakiwemo madaktari ni wanawake na leo ni siku muhimu ya Wanawake Duniani huduma zote zinatolewa bure kwa siku ya leo na madaktari wanawake nawaomba wananchi wa Wilaya ya llala na pembezoni mfike kupata huduma bure asubuhi mpaka jioni," alisema Dkt.Kiwelu.
Dkt.Kiwelu alisema huduma zote siku ya leo zinatolewa na wauguzi na madaktari wanawake kutibu magonjwa mbalimbali.
Aidha, Dki.Kiwelu alisema mikakati ya hospitali hiyo kujenga jengo la kisasa la kusafisha damu michakato yake imeanza rasmi.
Source: Majira