Asilimia 90 ya mahusiano bora yanajegwa kwa misingi ya kuvumiliana na kubebeana madhaifu, huyo ndio maana ya upendo

Kwa sisi tulio oa, tumekuelewa sana. Uvumilivu ni jambo zito sana ila ni tiba mona kubwa sana na yenye tija isiyo kifani.

Vijana wengi hili hawalijui, unakuta kijana anamtaliki mkewe au mke abaomba talaka kwa jambo ambalo tukilipima katika mizani ya haki, si sababu ya kufanya watu waachane. (Hapa naongelea khasa kwenye ndoa, mahusiano nje ya ndoa, nawaachia wahusika).

Lakini kadhalika kuna mambo hayavumiliki katika ndoa, haya yakitokea lazima mke aachwe tu au mke aombe Talaka. Miongoni mwa mambo yasiyo vumilika ni mke au mume kuwa MSHIRIKINA.

Narudi....
 
Uvumilivu ktk ndoa ndio kila KITU...lakin lililokuu NI KUMCHA MUNGU....NA HAKIKA KTK NDOA YANGU ISINGEKUWA UVUMILIVU WA MKE WANGU(MUNGU AZIDI KUMBALIKI)tusingekuwa hapa tulipo....UPENDO UMEBEBA KILA KITU,
UKIMPENDA
utamjali
Utamvumilia
Utamheshimu
Utamsikiliza(wengi tunasikiliza marafiki zetu)
Nk
 
Si kila kitu ni cha kuvumilia,mfano Mimi ni Samsoni ambaye Mungu amenikataza nisinyoe nywele kamwe halafu anatokea Delila in the name of love ananifanyia Manipulation halafu baadae ajenda yake inageuka kunishurutisha nimpe siri ya nguvu zangu au ninyoe nywele kinyume na Mungu alivyoniagiza na mbaya zaidi ananitishia kabisa eti kama hunyoi nywele mimi na wewe basi. Yaani hapo kwa kumsaidia sana nitamsindikiza kabisa. Aende tu.
 
Ahsante Kwa muongozo...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…