Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Vijana vijana vijana! Nimewaita mara 3 kumbe hali ndiyo ipo hivi kuwa umiliki wa video za ngono ni mkubwa kuliko kumiliki maarifa mazuri na pesa. Mbona hii ni balaa sana!
===================
Imeelezwa kuwa zaidi ya asilimia 95 ya vijana nchini wameathiriwa na ukuaji wa kasi ya teknolojia ya mtandao na kupenda kufuatilia mambo yasiyofaa kwenye majukwaa ya mitandaoni hususani picha za ngono na masuala yahusuyo ngono kuliko mambo ya msingi.
Hayo yamebainishwa na Mwalimu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano, Joyce Kisha wa huduma ya Daughters and Son's of Jerusalem Ministries jijini Dodoma wakati wa Kongamano la Vijana ambapo amesisitiza vijana kuacha kutumia mitandao vibaya kiasi cha kuharibu saikolojia zao na kupoteza mwelekeo wa maisha.
"Siku hizi kwenye TikTok kuna watu wanaweka live streaming lakini anataka kuwashawishi vijana, labda anajiweka anavyotaka yeye mwenyewe, mtu unaweka bando unajiunga kwenye hizo live, ili tu uangalie msichana anacheza akiwa uchi, inakufanya unakuwa na hamasa ya kufanya ngono akili inadorola unafikiri utafika?" amesema Mwalimu Joyce.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Challity Kichona amesema vijana wengi akili zao zimeshaharibiwa kutokana na kuendekeza mambo yasiyofaa ambayo hutokea ulimwenguni ikiwemo kuwapa kipaumbele watu maarufu wanaofanya matendo yasiyokuwa ya mfano wa kuigwa katika jamii
Kongamano hilo limeenda sambamba na uzinduzi wa tovuti ya Daughters and Son's of Jerusalem Ministries ambayo itakuwa inachapisha mafundisho mbalimbali yahusuyo vijana.