Asilimia 98% Simba SC wanaamini watapindua matokeo

Asilimia 98% Simba SC wanaamini watapindua matokeo

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,039
Reaction score
5,560
Moja kwa moja kwenye mada.

Hawa Simba yaani bila kupepesa macho kwenye akili zao wanaamini kabisa kesho watapindua meza na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika. Come on guys magoli 4 ni mengi sana, mlikosea sana ile mechi ya kwanza. Mechi ya kwanza mlijiamini sana pia mkawa na dharau kwa Chiefs.

Binafsi naamini simba hapo kesho atashinda ila sio ushindi wa 4 bila ama 5 bila hiyo kitu haito tokea. Jana nimeona na kusikia Manara akisisitiza kuwa lazima washinde tena ana mzuka kabisa huku anatikisa miguu jicho kavu limemtoka balaa.

Ukweli ni kuwa first leg mliwadharau sana Chiefs.
 
Kuna mmasai leo kaacha watu hoi sana. Anadai Simba inashida 7-0 kesho afu anaongea kwa kujiamini sana mpaka ameweka 20k kwa buku watu wakapgopa.
Nimecheka aisee, mwenyewe apa kuna chalii mimemuambia weka 10k kwa 30 kaguna

Wanasimba tuna moyo wa matumaini sana
 
Yaani Simba wanaamini kabisa wameisha tinga nusu fainali, kuna sheikh jana nimemsikia Clouds FM anasema yuko kwenye mfungo na maombi akiamin Simba atashinda goli 7 kwa sifuri. Kisha atachinja ng'ombe 7 sijui ndio nini hiyo.
 
Hadi sasa leo ijumaa tayari Simba inaongoza kwa goli 2:0

Maana Kaizer wameshamuogopa Refa aliyepangwa toka kwa majirani zetu, kisha wanaogopa habari za kupima Covid wameshajipima kwao kabla ya kuanza safari kwa woga wa fitna.

Je, kesho wakikuta majivu tu pale uwanjani si wataogopa hata kuingia vyumbani kwa woga? Kumbe mbwembwe na mikwara ya nje ya uwanja ni silaha tosha.
 
Simba kule kujiamini kupita maelezo kuna waponza sana pia na yule mpuuzi wenu anawaaminisha ujinga akiwa kwenye vyombo vya habari. Leo hii imefikia mashabiki wa simba wanaamini kabisa timu yao ikiwa uwanjani lazima ishinde kumbe mpira hauko hivyo. Ipo siku mtakufa kwa kuamini ujinga.
 
Hatupindui meza ila tumefika robo fainal ya club bingwa, nyie utopolo mtuambie lini mtafika huku. Au mtabaki kuongerea habari za Simba tuu
Itafika tena zaidi ya robo fainali, ikifikia mfumo kama unaoendeshwa na Simba
 
Hadi sasa leo ijumaa tayari Simba inaongoza kwa goli 2:0

Maana Kaizer wameshamuogopa Refa aliyepangwa toka kwa majirani zetu, kisha wanaogopa habari za kupima Covid wameshajipima kwao kabla ya kuanza safari kwa woga wa fitna.

Je kesho wakikuta majivu tu pale uwanjani si wataogopa hata kuingia vyumbani kwa woga?. Kumbe mbwembwe na mikwara ya nje ya uwanja ni silaha tosha.
Hizo zinaitwa mind game mkuu. Kumbuka first leg ilikuwaje, jamaa wakasema wana wacheza injury kibao, halafu wakawapa sifa timu ya Simba halafu wakajiweka kwenye unyonge. Kilichotokea ni goal nne. Hapa wanawapa tension marefa na pia wapimaji.
 
Kwa kipindi hiki timu yoyote ya Tz ikicheza na Kaizer haitakiwi kwenda kushambulia ni kwenda kujificha na kutegemea kaunta au mashuti ya nje ya box na kurudi kujificha.

Wazia fainali ya FA ya Leicester na Chelsea.

Kocha huwezi kua kama Wenger au Klopp wewe game plan yako ni kushambulia tu hujui unayekutana naye leo kakuacha mbali.
 
Asilimia 98 upotolo kuanzia mdhamini, viongozi na wqchezaji wao wanaamini yanga atakuwa bingwa hebu tuzungunzie kwanza hilo.
 
Moja kwa moja kwenye mada.

Hawa Simba yaani bila kupepesa macho kwenye akili zao wanaamini kabisa kesho watapindua meza na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika. Come on guys magoli 4 ni mengi sana, mlikosea sana ile mechi ya kwanza. Mechi ya kwanza mlijiamini sana pia mkawa na dharau kwa Chiefs.

Binafsi naamini simba hapo kesho atashinda ila sio ushindi wa 4 bila ama 5 bila hiyo kitu haito tokea. Jana nimeona na kusikia Manara akisisitiza kuwa lazima washinde tena ana mzuka kabisa huku anatikisa miguu jicho kavu limemtoka balaa.

Ukweli ni kuwa first leg mliwadharau sana Chiefs
Mzulu atakeketwa mchana kweupeeeeee
 
Huyo Manara ndio huwa anawapoteza Simba...
anawafanya Simba wajione Barcelona kumbe ushuzi tupu.....
Ushuzi ndo huo upo robo fainali...
Ushuzi ndo huo una Ubingwa 4 yrs..
Kama SSC ni ushuzi Utopolo ni nini?
 
Back
Top Bottom