SoC03 Asilimia hamsini (50%) huduma za maji na umeme

SoC03 Asilimia hamsini (50%) huduma za maji na umeme

Stories of Change - 2023 Competition

MTWARA- GAS CITY

New Member
Joined
Jun 21, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Maji na Umeme vimekuwa vitu muhimu katika maisha ya binadamu pia kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Gharama ya Maji na Umeme ni kubwa sio tu katika usambazaji yaani serikari pia kwa mtu mmojammoja anapohitaji kufungiwa inakuwa ni kikwazo.

CHANGAMOTO
Gharama za mwanzo za ufungaji wa maji na umeme

MATOKEO YA GHARAMA ZA MAJI NA UMEME
Uharibifu wa miundombinu, kama vile kupasua mabomba.
Wizi na vishoka,
Kupotea kwa mapato ya taifa,
Matumizi ya maji ambayo si salama yanayopelekea magonjwa mbalimbali.

SULUHISHO
Nashauri wizara kusika na serikari kwa ujumla kutoa huduma za ufungaji (Installation) Maji na Umeme bure au nusu ghararama (50%)

Maji au Umeme itamfikia kila mwananchi bila kuhitajika kulipia kwanza baada ya kufungiwa kila unit ya matumiz yake ikatwe asilimia fulani, kwa mfano mtu anaponunua umeme wa 1000 shilingi 100 ikikatwa kulipia gharama za Installation mpaka pale atakapomaliza jumla ya gharama alizokuwa anatakiwa alipe.

Mpenda maendeleo.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom