Uchaguzi 2020 Asilimia kubwa ya waliofananishwa na ng'ombe wasio na mkia huenda wakapigwa chini mchakato wa kupitisha majina ya wagombea utakapoanza

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwa mtu mwenye kufikiri kwa kina na kujiuliza mara kadhaa kabla ya kufanya uamuzi,ni wazi angeitumia kauli ile ya watu kufananisha na ng'ombe wasio na mkia kama hatari au ishara ya hatari kukubali kuwa ngo'mbe mpya asie na mkia mara tu baada ya kauli ile kutoka

Mpaka sasa sitaki kuamini kama muhusika alikuwa anatania na kwamba sasa amesahau kauli ile bali naamini anasubiri wakati muafaka ufike ndio aitekeleze kwa vitendo.

Kutekeleza kauli ile kipindi hiki itakuwa ni sawa na kuhujumu jitihada za kubomoa upinzani kwani itawakatisha tamaa ng'ombe wapya wasio na mkia kuingia zizini hivyo wataachwa waingie kwa wingi tu kipindi hiki.

Ukweli ni kwamba thamani ya hawa waliofananishwa na ngo'ombe asie na mkia ni pale tu wawapo nje ya zizi ila wakishaingia zizini, thamani yao hupoptea/hushuka.

Wasubiri kutoswa wakati utapofika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…