Asilimia kubwa ya wanawake kwenye baa kwa sasa wanajiuza, zamani ilikuwa tofauti

Asilimia kubwa ya wanawake kwenye baa kwa sasa wanajiuza, zamani ilikuwa tofauti

Caps Lock

New Member
Joined
Apr 28, 2021
Posts
2
Reaction score
2
Wakati nilipokuwa shuleni sekondari o-level enzi hizo pale Tanga Tech, japo ilikuwa ni bweni na ukali wa head master Mr Teti, mara kadhaa mimi na marafiki zangu tuliweza kutoroka na kutinga sehemu za starehe kama Raskazone Beach ama club LacasaChika kwa ajili ya kuburudika kimziki. Huko tulikutana warembo watoto wa shule ya Eckenforde waliotoroka mahosteli na kuja kujichanganya mjengoni (La Casa).

Ilikuwa ni sound zako na muonekano wako yaani unadhifu (pamba kali) ndio ulivutia warembo unapata mchuchu wa kuserebuka naye kwenye dance floor mpaka majogoo, ukiwa domo zege utaambulia kushika mapembe tu. Kimbembe ilikuwa namna ya kurudi shuleni asubuhi, enzi hizo za adolesence wasichana walitupendea kwa muonekano wetu na kujiamini tu haikuwa sana mambo ya fedha. Nilichomoka pale TTS na division one yangu safi na kuchaguliwa kuingia A-level shule ya Old Moshi.

Tulivyokuwa A level pale Moshi mjini na mwanangu JT niliendelea na kutembelea club kama kawaida club kama Pub Alberto, Laliga na Malindi ndio zilikuwa na umaarufu, tulitinga viwalo vyetu na kuzama pande hizo mimi na mwanangu JT. Haikuwa jambo la ajabu kutoroka shule kwa sababu shule haikuwa na uzio, japo tulichukua mchepuo wa PCM hatukuacha kula bata siku moja moja hasa weekend na haikutuathiri kimasomo kwani mwisho wa siku tulifaulu wote kwa division one na kujiunga na chuo kikuu cha UDSM.

Wakati fulani wa likizo nilimtembelea aunty yangu huko Arusha lakini kuna mara kadhaa nilimuomba ruhusa kukaa na marafiki zangu waliokuwa wakisoma pale Arusha Technical College na hapo nilipata mwanya wa kuzama club Triple A, na mpango ulikuwa ni ule ule kupendeza na sound zako unang'oa mchuchu wa kucheza naye muziki, mitungi haikuwa kwa sana japo nilikuwa napiga kidogo bia mbili tatu, sigara hapo sikujaribu kabisa, niliogopa mama alinionya kwamba nikijaribu basi nitapata kifua kikuu na bangi akaniambia nikijaribu nitakuwa kichaa basi nikabaki na mwendo wa bia ama soda tu nikikosa kabisa maji baridi.

Nilipochaguliwa kusomea Computer Science na rafiki yangu JT pale chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) hatukuacha asili yetu ya kula bata siku moja moja, club Billcanas ilikuwa yamoto bila kusahau club Maisha ilikuwa pale Oysterbay. Tulivyopokea boom letu la kwanza na kupewa mkononi ili kufungua akaunti, (miaka hiyo ilikuwa boom la kwanza unapewa mkononi) tulizama UDASA (club ya maprofesa pale UDSM) tukapiga mitungi yetu na kisha tukarudi kusumbua wana pale hall 5 floor ya kumi. Washkaji walitushangaa namna tulivyo adapt mazingira fasta tu.

Nakumbuka siku ya bash (sherehe ya kupokea first year) muziki ulipigwa pale ukumbi wa Nkrumah, sikuondoka mikono mitupu, nilikuwa nimenyuka pamba za maana za kichuga chuga jeans plane modle na Tshirt na kikoti juu na raba yangu mpya Airforce One nilinunua sokoni Memorial, sikusahau unyunyu. Basi ile kucheza mziki tu naona mrembo huyo wa firsy year mtoto kutoka Mwanza, Nyegezi, nikakamatia mpaka muziki unafungwa nikamsindikiza namshusha ngazi za pale Nkrumah na kumpeleka mpaka hall 7.

Sikuhiyo sikuondoka mikono mitupu niliambulia kiss na romance na ahadi kibao, ndio ilikuwa mwanzo wa kuwa na mahusiano ya chuo lakini guess what? Haya mahusiano ya hayakudumu nilipigwa kibuti nilipomfuma na boy mwingine nikalia kama mtoto na kuahidi kutopenda tena mtoto wa chuo. Washkaji walinizunguka na kuniasa tulishuka pale Ubungo na kuzama Yenu Bar nililewa na kurudi room kujipanga na UE sikutafuta tena mrembo wa chuo mpaka nilipo hitimu.

Kipindi hicho ukizama club kama Bills au maisha O'bay unaweza kupata watoto wa IFM ama watoto wa Magogoni kirahisi kwa saund zako tu, mahusiano hayo yalikuwa msingi wa kufikia kwenye ndoa, wapo washkaji kibao nawajua walipata wenza wao kwa njia hii huko maclub na huko kwenye ma University bashes. Lakini siku hizi mambo yamebadilika, baada ya club zote hizi kufa yameibuka mabar ambayo vijana wanakesha wakinywa pombe na asilimia ya wanawake walioko huko ni wale walio shindikana.

Huwezi kupata wadada wa maana na warembo wanao nukia uturi kwenye pande hizo, wengi ni wale wenye UTI sugu na wapo kibiashara ukimsalimia tu unasikia "una sh' ngapi?" "show time ama tunalala?!" Kwa hivyo kujenga mahusiano kwa vijana wa sasa imekuwa vigumu kwa sababu ni vigumu kumpata mwanamke wa ndoto zake kwenye sehemu za starehe ama kwenye night clubs wengi wameishia kutapeliwa kwenye mahusiano ya aina hii. Maisha yamebadilika.

Msinielewe vibaya wakuu nimejaribu kushare experience tu.
 
Back
Top Bottom