tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Hata Mimi nasubiri ndipo utaona bora ukutane na Simba msituni na siyo binadamuNasubiri comments za wanachadema🤣
skari 15 waliopo mafunzoni katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi, maarufu zamani kama CCP mkoani Kilimanjaro, wamenusurika kifo baada ya gari walilopanda kuhusika kwenye ajali ya uso kwa uso na lori aina ya Fuso.
Tukio hilo lilitokea jana, Jumanne Agosti 12, 2025 katika eneo la Kwa Sadala, Wilaya ya Hai, likihusisha gari la polisi lililokuwa likitoka kambi ya jeshi la polisi wilayani Siha na lori hilo lililotokea upande wa Moshi.
Soma pia: Askari afa kwenye ajali ya gari njia ya Chanika. Alikuwa kwenye gari dogo lagongwa na daladala
View attachment 3439999
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa majeruhi wote wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Hai kwa matibabu.
Alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano asubuhi, baada ya gari aina ya Landcruiser la jeshi la polisi kugongana uso kwa uso na lori la Fuso, na kusababisha majeruhi kadhaa.
RC Babu aliongeza kuwa magari hayo yalikuwa yakitokea pande tofauti; gari la polisi likitoka Bomang’ombe kuelekea mjini Moshi, likiwa limewabeba wanafunzi wa jeshi la polisi kutoka kambini, huku lori la Fuso likiwa kwenye shughuli zake za kawaida likitokea Moshi.
Alisema chanzo kamili cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na vyombo husika.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Dk. Emmanuel Minja, amesema walipokea majeruhi 15, ambapo mmoja kati yao amepewa rufaa kwenda Hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi.
Alibainisha kuwa hali za majeruhi wote zinaendelea vizuri, huku baadhi yao wakishonwa majeraha na kupatiwa huduma ya kwanza haraka baada ya kufikishwa hospitalini.
Chanzo: Global online tv
Kwani wamekufa wana CCM?Nasubiri comments za wanachadema🤣
Sasa ni kwa nini HAWAKYFARIKI?skari 15 waliopo mafunzoni katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi, maarufu zamani kama CCP mkoani Kilimanjaro, wamenusurika kifo baada ya gari walilopanda kuhusika kwenye ajali ya uso kwa uso na lori aina ya Fuso.
Tukio hilo lilitokea jana, Jumanne Agosti 12, 2025 katika eneo la Kwa Sadala, Wilaya ya Hai, likihusisha gari la polisi lililokuwa likitoka kambi ya jeshi la polisi wilayani Siha na lori hilo lililotokea upande wa Moshi.
Soma pia: Askari afa kwenye ajali ya gari njia ya Chanika. Alikuwa kwenye gari dogo lagongwa na daladala
View attachment 3439999
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa majeruhi wote wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Hai kwa matibabu.
Alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano asubuhi, baada ya gari aina ya Landcruiser la jeshi la polisi kugongana uso kwa uso na lori la Fuso, na kusababisha majeruhi kadhaa.
RC Babu aliongeza kuwa magari hayo yalikuwa yakitokea pande tofauti; gari la polisi likitoka Bomang’ombe kuelekea mjini Moshi, likiwa limewabeba wanafunzi wa jeshi la polisi kutoka kambini, huku lori la Fuso likiwa kwenye shughuli zake za kawaida likitokea Moshi.
Alisema chanzo kamili cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na vyombo husika.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Dk. Emmanuel Minja, amesema walipokea majeruhi 15, ambapo mmoja kati yao amepewa rufaa kwenda Hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi.
Alibainisha kuwa hali za majeruhi wote zinaendelea vizuri, huku baadhi yao wakishonwa majeraha na kupatiwa huduma ya kwanza haraka baada ya kufikishwa hospitalini.
Chanzo: Global online tv
Tambua ya kwamba, Uovu, udhalimu na Uhalifu ambao umekuwa ukifanywa na Watu hao hauchagui itikadi za Vyama, makabila, au kigezo kingine chochote kile. Hata wao kwa wao pia wamekuwa wakifanyiana Uovu, wanaolengwa zaidi na Uovu wao ni wale baadhi ya Askari Polisi wachache ambao ni Wapenda Haki na kupinga uonevu na udhalimu. Rejea tukio la Mauaji ya makusudi ya yule Mfanyabiashara wa Madini kule Mtwara, yule Askari Polisi aliyekuwa Muadilifu na aliyefichua Mauaji yake wenzake (wakubwa wake) walimkamata na kumuweka rumande kwenye Kituo Cha Polisi, na mida ya usiku yule Askari Polisi aliuawa kwa kunyongwa na kisha watekelezaji wa tukio hilo asubuhi walitoa taarifa kwa umma kwamba eti Askari Polisi huyo alijinyonga kwa dekio akiwa katika Mahabusu ya Polisi!Nasubiri comments za wanachadema🤣
CHADEMA tunawapa pole wahanga wote wa ajali tunawatakia na kuwaombea uponyaji mwema na wa haraka.Nasubiri comments za wanachadema🤣
Umenifurahisha sana binti cocastic. Hata wewe? Sikutegemea🤣Kwani ibilisi siku hizi ana majukumu gani mengine ya maana, hadi asiwepo eneo la tukio na kuwajibika ipasavyo?
Mie ananiudhi, 😂😂😂😂
Naunga mkono hojaDuh! ningekuwa karibu ninge.....