Askari 19 wa Wanyamapori kizimbani madai kuomba, kupokea rushwa

Askari 19 wa Wanyamapori kizimbani madai kuomba, kupokea rushwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana na Kikosi Kazi Taifa Dhidi ya Ujangili, imewafikisha mahakamani askari 19 wa wanyamapori kwa tuhuma za rushwa.

Watuhumiwa hao wakiwamo askari wa Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. milioni 70.4 kutoka kwa wafugaji wa maeneo ya Itilima mkoani hapa

Kati ya watuhumiwa hao 19, watatu ni watumishi wa kampuni ya uwindaji ya Fredikin Conservation Fundi (FCF)

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Joshua Msuya, alisema watuhumiwa hao walisomewa mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Simiyu, Venance Mlingi.

Alisema watuhumiwa hao walisomewa kesi tano za rushwa tano ambazo kati ya hizo tatu ni namba 14, 15 na 16 za mwaka 2020 chini ya Hakimu Mlingi na kesi mbili namba 17 na namba 18 mbele ya Hakimu Marry Nyangusi.

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Kelvin Murusuri, alidai kuwa kati ya Aprili Mosi na Juni 30, mwaka huu, watuhumiwa hao kwa tarehe tofauti, kwa pamoja walikamata watu na mifugo yao waliyokuwa wakiichunga ndani ya pori la akiba la Maswa na kuwaomba rushwa ili wasiwachukulie hatua za kisheria.

“Watuhumiwa kwa pamoja na kwa nyakati tofauti waliwaomba watu hao rushwa, ili wasiwachukulie hatua kwa kuwa walikuwa wakichunga ndani ya hifadhi la pori la Maswa na waliomba kupewa Sh. 30,000 hadi 70,000 kwa kila kichwa cha ng’ombe waliokamatwa,” alidai.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa katika mashtaka waliyosomewa, watuhumiwa waliomba na kupokea Sh. milioni 70.4 kutoka kwa wafugaji waliokamatwa.

Watuhumiwa waliosomewa mashtaka ni James Chacha, Janeth John, Derick Mboneko, Baraka Lunengo, Anthony Hosea, Henry Kwambaza, Hombo Bajuta, Joseph Pius, Flavian Magabari na Kelvin Jackson.

Wengine ni Chacha Mwita, Magomba Mkaka, Juma Peter, Yohana Mkanzabi, Omari Katongari, Elibert Temba, Leonard Kileo na Maridadi Maridadi.

Watuhumiwa wote walikana mashtaka na wamerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana na kesi zao zimeahirishwa hadi Septemba 15 na 19 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa baada ya upelekezi kukamilika.

NIPASHE
 
Back
Top Bottom