Askari 8 wanashikiliwa Morogoro kwa tuhuma za Mauaji ya Ally Zona

Mlyafinono

Senior Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
177
Reaction score
47
-Habari zilizotufikia punde ni kwamba askari wanane (8) wamekamatwa mkoani Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya Muuza magazeti Ali Zona wakati wa maandamano ya Chadema yaliyofanyika mwezi uliopita mjini humo.

-Mjini Iringa mtuhumiwa wa mauaji ya Daudi Mwangosi hakuweza kufikishwa mahakamani leo kama ilivyokuwa imepangwa.

-IGP Mwema bado yupo Iringa anahaha kuzungumza na viongozi wa dini kusaidiwa kupoza mambo katika jamii kuhusu tukio la kuuawa kwa mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, tukio ambalo limeonekana kugusa hisia kali miongoni mwa wanajamii mkoani humo.
 
Hivi kwani wauaji si wanaonekana katika picha zote za still na video. Sasa inakuwaje bado hawajapanda kizimbani? Mbona ya Kanumba Lulu alipanda mahakamani immediately wakati hata haijulikana alisukuma mtu au vipi? sasa this glaring action and event sasa mnasema nini polissmmmmmm nyie?
 
Kwanini wanawakamata hao kabla ya TUME huru kuundwa, wakati Nape alisema Tundu Lisu ni muongo amedanganya umma kuwa POLISICCM ndiyo waliofanya mauaji. Wanatafuta mbinu ya kuwavisha watu makosa, wakati kama kungekuwa na TUME huru tungejua kwa undani kwamba hawa askari walipewa maagizo gani, na nani, na kwaajili ya nini?
 
Enyi Makamanda wenzetu CHADEMA,

kama mlikua hamna taarifa ya yale yanayoendelea nyuma ya pazi hadi hivi sasa ukweli wa mambo ni kwamba SERIKALI YA RAIS KIKWETE hadi hivi sasa
imebanwa to the maximum (unaweza ukarudia hilo fungu la maneno mara 10 ukipenda) kufuatia huu mlolongo mrefu wa UKATILI WA JESHI LA POLISI DHIDI YA RAIA NA CHADEMA ...

... hot hot zaidi ziko njiani huku baadhi ya vingunge wana-CCM wakitupiana mpira kushoto kulia. Kaeni mkao wa kula juu ya haya.

Hilo ndilo neno la leo huku tukimwambia Mze Wasira, Nchimbi pamoja na Mwema kwamba mbele ya kitu 'HAKI YETU' katu haturudi nyuma hatubanduki hata kwa mizinga!

Mabadiliko ya kweli yaja tena hayazuiliki hata kwa dawa!!
 



Asanteni Kamati Kuu CHADEMA walau kwa kuitikia sauti ya na majonzi ya umma wa Tanzania na kutoa dira kwa Taifa, kukemea na kuainisha mambo gani yafanyike ili kutokomesha UKATILI WA JESHI LA POLISI dhidi ya raia na mauaji yasiokwisha kila kona ya nchi.

Hakika bado tunaomba sana mambo yasiishie tu hapo kwenye ma-tamko bali zaidi wananchi tunaasubiri kuona CHADEMA kinavyofwatilia utekelezaji wa kila agizo la Kamati Kuu taifa kwa faida yetu sisi walalahoi huku vijijini.

Elimu ya uraia kwa umma wa Tanzania sasa ndio iongezewe kasi maraduru ili kila kijiji kiweze kufikiwa ki-undani zaidi na zaidi.


 
Last edited by a moderator:

Mbona jana hujatuambia nini kimezunguzwa katika kikao cha wauaji wa watanzania wanaotumia unifomu za polisi? Hivi huyo Shemeji wa Vasco ndio mtuhumiwa nambari wani
 
Kumbe ile ishu ya UNDEFINE FLYING OBJECT (UFO) ilitokea kwa polisi. Ile Ilikua ni mbinu dhaifu.
 
Jamani yule Senso wa Polisi makao makuu yu wapi na majibu yake ya kufikirika kwenye njozi??tunamtaka atupe tena majibu ya kilichoomuua Mwangosi!!
 
kama kweli tunashukuru kwamba hatua zimeanza chukuliwa, lakini tatizo ni ajira zisizo fuata uweledi, watoto watukutu ndio wanao ajiriwa polisi
 
Wakuu hivi huyo muzungu kwenye picha ni nani? Kweli hili chama ni balaa limedhihirisha ni la wote hakuna ubaguzi wa aina yoyote iwe dini, rangi, jinsia, wala nini. Viva Chadema.
 
Jk nchi haitawaliki ndo hivi mwanakwetu
 

Mkuu, nimetamani sana kujua yaliyomkuta dada yetu huyo. Bahati mbaya natumia simu. Please help!
 
Hilo ni igizo lingine. Hakuna la maana. Cha kujiuliza hapa ni kwamba iweje washtakiwe wakati tume haijamaliza kazi! Ikija na majibu tofauti? Its another silly season! Au series kama Isidingo.
 
Hakuna kurudi nyuma,JUSTICE MUST PREVAIL!Na huu ndo uwe mwisho wa udhalimu.Kama kwenye process hiyo ukombozi utapatikana,basi na iwe hivyo.
 
Hapana,askari wanaonewa,wao hutekeleza maagizo tu na ndicho walichoapa.Wauaji ni wale wanaotoa maagizo haya.Hawa ndio wanaostahili kukamatwa na kukatwa shingo zao.Inauma sana machozi yanitoka
 
Mbona jana hujatuambia nini kimezunguzwa katika kikao cha wauaji wa watanzania wanaotumia unifomu za polisi? Hivi huyo Shemeji wa Vasco ndio mtuhumiwa nambari wani

Kweli somo la historia ni adimu tena kwa watu wengi tz. I wish'you'could hv little of knowledge of what is so called wind of change; its sweeping tz now and its accelarated by people like you who do not turns blind'eye'from reality. chadema wameua wapi for heaven sake point out. Shame on you!
 
Mbona wanawaacha wahusika halisi Mwema na Nchimbi na kuwaonea hawa wanaopokea amri zao tu na hawatakiwi kuzipinga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…