Askari amstua Hakimu kwa kuwa Shahidi upande wa Mshitakiwa

Askari amstua Hakimu kwa kuwa Shahidi upande wa Mshitakiwa

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
SAKATA la wizi wa gari aina ya RAV4 lenye namba za usajili T. 984 BPG, limeendelea kuibua mapya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, baada ya askari polisi J 212 PC Damas kutoka Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni kutoa ushahidi akiwa upande wa mshtakiwa.

Wakati Damas anatoa ushahidi wake kwa kumtetea mshtakiwa Salum Mshana, tayari baadhi ya askari, akiwamo mpelelezi wa kesi hiyo walishatoa ushahidi wao kwa upande wa mashtaka kwa lengo la kuthibitisha wizi wa gari hilo.

Hali hiyo ilitokea juzi mbele ya Hakimu Mkazi, Aaron Lyamuya wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji wa mashahidi wa upande wa mashtaka, ndipo askari huyo alipopanda katika kizimba cha shahidi.

“Sijawahi kukutana na kitu kama hiki - polisi kuja kuzungumza kwa upande wa utetezi. Siyo kusema kwamba inakatazwa, hapana! Inaruhusiwa kabisa.

“Haya, sawa ngoja tumsikilize. Sasa sijui utazungumza nini wakati wenzako walishazungumza kwa upande wa mashtaka. Haya mwapishe tuanze,” alisema Hakimu Lyamuya.
 
Back
Top Bottom