Askari kuvaa kiraia huku wakiwa mamebeba silaha si sahihi

rushanju

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
3,238
Reaction score
5,106
Wakati wa shambulio la Bw. Hamza, tumeona watu wengine kwenye eneo la tukio wakidhani Hamza ni Askari. Hii imekuwa kawaida kuwavalisha Askari wetu nguo za kawaida harafu mnawapa bunduki.

Inasemekana mmoja wa Askari alijeruhiwa na Askari wenzie maana alikwa na bunduki bila ya sare. Juzi nimekutana na Askari pale Muhimbili mortuary akiwa kavaa kiajabu sana lkn mkononi ana Said Maulid (SMG) nikajiuliza maswali mengi sana, sikupata jawabu.

Inapotokea kwenye mashambulizi kama like la juzi, si mtazibuna wenyewe kwa wenyewe? Jukumu la ulinzi pia ni letu sisi kama raia.

Sasa tutajuaje huu upuuzi. Ikitokea piga nikupige kama ya juzi nami niko jirani na shotgun yangu nawe ukanipita jirani na SMG bila nguo si nakufumua tu. Wazee wa Intelijensia naomba mjitathimini sana

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Friend fire. Kuna jamaaa pale getini aliyevaa shati jekundu alitaka kummalizia yule jamaaa aliyepigwa risasi za mguu na Hamza, wenzake wakamuwahi kumtuliza.
 
Hii ndiyo bongo,askari kanzu ni kama majambazi,eti sabaya nae alikua na askari kanzu, kumbe ni majambazi.

Hata hawa ndo wanachofanya,anapewa silaha kwa nia njema,yy anaenda kutisha raia na kupora ama kulazimisha kupewa kitu kidogo.

Too sad
 
Mi nafikiri watafute njia nyingine ya Siri ya utambulisho wao wenyewe mf. Wanaweza vaa kapelo kwa dizaini flani hivi ambayo wenyewe wanaitambua kuliko kutaka kumwagana ubongo wenyewe kwa wenyewe.
 
Wakati wa shambulio la Bw. Hamza, tumeona watu wengine kwenye eneo la tukio wakidhani Hamza ni Askari. Hii imekuwa kawaida kuwavalisha Askari wetu nguo za kawaida harafu mnawapa bunduki.

Inasemekana mmoja wa Askari alijeruhiwa na Askari wenzie maana alikwa na bunduki bila ya sare. Juzi nimekutana na Askari pale Muhimbili mortuary akiwa kavaa kiajabu sana lkn mkononi ana Said Maulid (SMG) nikajiuliza maswali mengi sana, sikupata jawabu.

Inapotokea kwenye mashambulizi kama like la juzi, si mtazibuna wenyewe kwa wenyewe? Jukumu la ulinzi pia ni letu sisi kama raia.

Sasa tutajuaje huu upuuzi. Ikitokea piga nikupige kama ya juzi nami niko jirani na shotgun yangu nawe ukanipita jirani na SMG bila nguo si nakufumua tu. Wazee wa Intelijensia naomba mjitathimini sana

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Wapo wengi kama huyo mitaani muulize Nape

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom