Askari Magereza aliyesingiziwa kubaka ameachiwa huru

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,774
Reaction score
47,866
Hizi kesi tunazosomaga humu kwamba mtu mzima amebaka mtoto kumbe baadhi huwa ni za mchongo

Morogoro. Ofisa magereza katika gereza la Kingolwira mkoani Morogoro, Samwel Stanley, ambaye Agosti 22 mwaka 2022 alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa tuhuma ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka nane, ameachiliwa huru na Mahakama Kuu.

Hii ni baada ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Paul Ngwembe, kukubaliana na sababu za rufaa za mshitakiwa na ripoti ya uchunguzi mpya wa kisayansi uliothibitisha mtoto huyo alikuwa bado bikira.

Hayo yamo katika hukumu ya Jaji huyo aliyoitoa Januari Mosi mwaka huu na kupakuliwa katika tovuti ya Mahakama Kuu ya Tanzania (TanzLii) jana, huku akishauri upande wa mashitaka na wapelelezi kutumia sayansi kuthibitisha makosa.

Katika hukumu yake, Jaji Gwembe alisema katika kesi hiyo, mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa ushahidi kuwa alimnywesha mtoto huyo pombe kali aina ya K-Vant kabla ya kumbaka, lakini hakuna ushahidi wa kisayansi uliothibitisha hilo.

“Katika kesi hii upande wa mashitaka ulipaswa kujua mama wa mtoto ni ofisa tabibu akifanya kazi pamoja na PW 5 (shahidi wa tano wa Jamhuri), hivyo kulihitajika uchunguzi kutoka kwa mtaalamu huru,” alieleza Jaji Ngwembe.

Baada ya kumalizika kwa usikilizwaji wa pande zote katika kesi hiyo, Mahakama iliona kuna haja ya kufanyika kwa uchunguzi huru na pande zote ziliafiki na ndipo mtoto huyo akachunguzwa upya katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Uchunguzi
Hata hivyo, ingawa mahakama ilitaka pia mtoto achunguzwe kama kuna wakati wowote aliwahi kutumia kilevi, lakini Dk Deodata Ruganuza aliyefanya uchunguzi alisema hilo lisingewezekana kwa kuwa ulikuwa umepita zaidi ya mwaka.

Katika ripoti ya uchunguzi ya Dk Ruganuza, alisema kama mtoto huyo wa miaka nane angeingiliwa na mtu mzima, ni lazima kungekuwa na mikwaruzo na pia bikira isingekuwepo kwa kuwa ikishaondoka huwa haiwezi kujitengeneza tena.

Jaji awashukia wapelelezi

Jaji Ngwembe alisema kwa hekima anawashauri Jamhuri na wapelelezi kutumia utaalamu wa kisayansi kubaini ukweli wa tuhuma badala ya kumshitaki raia mwema na hatimaye kufungwa, kumbe tangu mwanzo hakutenda kosa hilo.

“Hii huwa ndio inaleta malalamiko kutoka kwa jamii kuwa wakosaji wa kweli kuna wakati wanaachwa huru, lakini raia wema wanajikuta wakisota gerezani. Katika nchi nyingi duniani, sayansi imesaidia mahakama kufikia hitimisho sahihi,” alisema na kuongeza kwa msisitizo:

“Kwa ujumla wake na mazingira ya rufaa hii pamoja na maoni kutoka kwa daktari bingwa wa wanawake, inathibitisha hakuna tendo la ubakaji lililofanyika kwa huyu mtoto ikiwa na maana hakuingiliwa na mtoto bado ni bikira.

Kutokana na hayo, Jaji Ngwebe alikubaliana na rufaa za mshitakiwa huyo aliyekuwa akitetewa na mawakili wawili, Neema Ndayanse na Damali Nyange na kufuta hukumu ya mahakama ya Wilaya ya Morogoro na kumwachia huru Stanley.

Hatima ya Stanley

Ofisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Magereza ambaye alikataa kutajwa kwa kuwa si msemaji, alisema baada ya hukumu hiyo, ofisa huyo anatakiwa kurudishwa kazini kwa hadhi aliyokuwa nayo kabla ya kupatikana na hatia na kufungwa.

“Unajua hili shitaka halina uhusiano wa moja kwa moja na kazi yake, kwa hiyo alivyoshitakiwa kipindi chote alikuwa akilipwa mshahara wake wote na ulikoma baada ya kufungwa ile Agosti mwaka jana. Kwa hiyo mahakama imemfutia tuhuma zile ni mtu safi kama alivyokuwa kabla ya kushitakiwa,” alisema.

Akizungumzia hukumu hiyo, Wakili wa Mahakama Kuu, John Mallya alisema kuwa mahakama imefuta ile kutiwa hatiani na adhabu, maana yake anatakiwa arudishwe kazini na kama alikuwa na cheo fulani basi atarudi katika cheo hicho kwa kuwa hakuna tena tuhuma dhidi yake na anarudi kama alivyokuwa kabla ya kushitakiwa.

Alivyotiwa hatiani

Kulingana na ushahidi uliomfunga ambao Mahakama imeufuta, tukio hilo lilidaiwa kutokea Jumapili ya Aprili 25, 2021 ndani ya kambi ya gereza la Kingolwira, iliyopo Mkoa wa Morogoro, ambako mshitakiwa na mama wa mtoto wanafanya kazi pamoja.

Akiwa nyumbani, mama wa mtoto alimuona mshitakiwa akiwa ameongozana na mwanawe wakitokea nyumbani kwa mshitakiwa wakielekea nyumbani kwa wazazi wa mtoto na mtoto alionekana amechoka na alikuwa akihitaji kulala.

Mshitakiwa, mwathirika (mtoto) na mama yake walikuwa wanaishi ndani ya kambi ya gereza hilo la Kingolwira lililopo mkoani Morogoro.

Ushahidi huo wa Jamhuri ukaeleza kuwa baadaye ilifahamika kwamba mtoto huyo alikuwa amepewa pombe kali aina ya K-Vant na mshitakiwa ambaye baada ya kumnywesha kilevi hicho, alimbaka na baadaye mama yake alipomchunguza, alimkuta ana damu na michubuko ukeni.

Akaamua kumpeleka kituo cha afya cha Kingolwira ambapo uchunguzi ulifanywa na tabibu mwingine anayefanya kazi katika kituo kimoja na mama wa mtoto aliyebakwa, ambaye alibaini mtoto huyo alibakwa zaidi ya mara moja.

Mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo upande wa mashitaka uliita mashahidi sita na kuwasilisha kielelezo kimoja, ambapo baadaye mahakama ilimtia hatiani ofisa huyo na kumhukumu kifungo cha maisha.

Hakuridhika kutiwa hatiani pamoja na adhabu hiyo, ndipo alipokata rufaa Mahakama Kuu kanda ya Morogoro, akiwasilisha sababu 11, ikiwamo kuwa mahakama iliegemea ushahidi wa kutengeneza wa kituo cha afya
 
Sasa hayo matundu ya kisheria yatazibwa na nani?

Kwa mfano ni hatua gani inayochukuliwa kwa mtu aliyemsingizia mwenzake na kumsababishia adhabu ya kifungo chote hicho?

Pili, ni hatua gani inayochukuliwa kwa hakimu anayehukumu kimhemuko kuharibu maisha ya wengine?
 
Inaonekana hakuna hatua yoyote imechukuliwa
 
Hizi kesi tunazosomaga humu kwamba mtu mzima amebaka mtoto kumbe baadhi huwa ni za mchongo

By Daniel Mjema
Mwandishi mwandamizi
Mwananchi Communications Ltd (MCL)

Jamaa maisha yake will never be the same again. Anachotakiwa kufanya ni kwenda kuanza maisha mbali kabisa nje ya mipaka ya nchi. Ikibidi aelekee zake Ituli au Kitchanga.
 
labia majora and labia minora mahakama inafundisha Biology sasa
 
Sasa hayo matundu ya kisheria yatazibwa na nani?

Kwa mfano ni hatua gani inayochukuliwa kwa mtu aliyemsingizia mwenzake na kumsababishia adhabu ya kifungo chote hicho?

Pili, ni hatua gani inayochukuliwa kwa hakimu anayehukumu kimhemuko kuharibu maisha ya wengine?
Dah!...walifanya uovu mbaya sana...inatakiwa wamlipe fidia.
 
Back
Top Bottom