ntagunga nimekuelewa, naku-regard kama miongoni mwa wahabarishaji wazuri!
Sikuchangia chochote kuhusu wanaharakati kwenye kadhia hii ya polisi kupigwa, lakini nikwambie sasa kuwa tukio hilo linalingana kwa maudhui kama si taathira, na maji kupanda mlima.
Tuwe na uelewa wa pamoja, Askari anapatiwa mafunzo mahsusi ya jinsi ya kutekeleza majukumu yake, kwa maneno mengine askari ni mtaalam wa saikolojia ya jamii angalau kwa mafunzo ya miezi 9.
Utaona wazi hapa polisi hakuwa mweledi vya kutosha ama alipuuza kwa maksudi au kwa msukumo wa kipato cha ziada, tahadhari ya "mob justice" ukijumlisha na maelezo yangu ya awali kuihusu gongo, utapata jawabu la hii "mob" ninayoi-refer kupambana na wanayemdhania kuwa mtunzi na mtia mkazo sheria wanayoiona kuwa kandamizi dhidi yao kwenye nyanja ya kiburudisho cha kilevi rahisi.
Ni kutokujitendea haki ikiwa tutadhani hili ni tukio la kupigiwa kelele na wanaharakati ambao wanauelewa wa kutosha kuhusu mamlaka, nguvu na wajibu walionao kisheria polisi wetu juu ya raia na mali zao.
Sisemi kuwa polisi wapigwe, la hasha, nasisitiza polisi kutumia taaluma yao preciously and positively.sheria na kanuni za kazi zizingatiwe, Kwa mfano ikitokea rabsha kwa wapenzi wa simba na yanga uwanja wa taifa, wakati simba inaongoza 4-0!!!!!!!!!! labda kamuhanda pekee ndiyo anaweza, lakini itakuwa ni kosa la mauaji kujaribu kutuliza rabsha hizo kwa mabomu ya mchozi kwenye uwanja uliofurika watazamaji zaidi ya 65,000. Likewise askari watatu kufanya jaribio la kukiarest kijiji kizima (hapa ni kwa mtizamo mpana) tegemea kuamsha jazba na munkari wa jamii husika.
Hapa uelewe hawa wananchi walikuwa wanafanya kama JWTZ ilivyofanya kwa idd amini alipovamia tanzania, ilikuwa kumpiga na kumtokomeza asionekane tena ili tishio lake litokomee pamoja naye,
walitaka huyu polisi asirudi tena au akome "kuwaonea" nimeutafsiri mtazamo wao.