Askari polis sengerema, apigwa kipigo cha mwizi, Hali yake ni mbaya.

wamekwenda kufanya kazi ambayo hakutumwa na wakubwa wao.
 

mkuu nimekusoma, umezungumzia uwajibikaji. Ni ukweli kabisa, kuna baadhi ya uhalifu unaendelea ni kwa kuwa tu POLISI nao hawataki kuwajibika kwa nafasi zao. Hilo halina ubishi.

sasa turudi kwenye mada. askari kapigwa akiwa anatekeleza wajibu wake, na amepigwa nusra ya kufa, je hana haki kwa sababu baadhi ya askari wanaendekeza rushwa katika utumishi wao? Je ni kweli anastahili kipigo hicho alichopewa kwa kisingizio polisi wenzake wanakula rushwa?

Na je nini nafasi ya wanaharakati, wanatetea haki za kundi fulani la watu huku makundi mengine wakiyaacha kwa sababu tu watu wa ofisini kwao wananuka kwa utumishi mbovu?
 

Story ni kwamba, walikuwa askari wawili na mgambo wawili kwa jishi nilivyoelezwa. Wqalipokamata ili kuwapeleka kituoni, wananchi wakawazingira kwa minajili ya kuzuia zoezi hilo. Kwa kuwa nguvu yao ilikuwa ndogo, wakaomba msaada kwa kiongozi wao ndipo alipowashauri waachane nao, na kama ni ukamataji utafanyika kivingine siku nyingine. baada ya kuwaachia likaibuka kundi lingine sasa likaanza kutoa kipondo, mmoja ndiye aliyeathirika zaidi.

Inawezekana hakuwa mwepesi, na inawezekana kuna tafrani ilitokea hata mimi sijui.

Lakini tuchukue taarifa ya awali kuwa polisi apigwa kichapo cha mwizi nusra ya kuuwawa. Je wanaharakati nini nafasi yao katika suala kama hili? vyombo vya habari isipokuwa JF, kwani ndiyo inatuwezesha kujadili jambo hili mbona hata haikusika? au haki zinawahusu kundi la watu baadhi tu? hili ndilo swala langu
 

ha ha ha ha, kwa hiyo polisi kisheria hakuna sehemu ya kumshtaki? yuko juu ya sheria? mi nadhani uko utaratibu wa kuwashtaki ingawa sijui vizuri. Kuna mwaka hapa mwanza polisi alipigwa na wanazengo, alipodai ni polisi wakambeba wakampeleka kwa kamanda wake, wanamwuliza, huyu ni askari wako? sijui ilimalizika vipi
 
tayari na wewe umeshaonyesha bias

nawapendelea polisi kwa kujaribu kudadisi nani mtetezi wa haki zao wanapodhulumiwa wakiwa katika kusimamia sheria na katiba ya nchi waliyoapa kuisimamia?
 
kosa moja halisahihishi kosa jingine, wanaharakati hawajaunga mkono askari kuumizwa, lakini askari kuua au kupiga raia ni mbaya sana kwa vile askari ana mafunzo maalumu na raia hawana na askari analipwa na kodi za raia hivyo askari alitakiwa atumie mbinu alizofundishwa kuwatoroka maadui kama wanavyoonyesha mbele ya mheshimiwa wakati wakihitimu mafunzo.
 
Asa maisha magumu watu hawana hela ya bia si bora wanye gongo glasi moja tu uko chakari
 

hacena sasa kama angekuwa na risasi hapo kungetokea nini mkuu. Na kwa kuwa yeye amepewa mafunzo ndo akipigwa asitetewe!!
 

kawaida na sheria inavyoelekeza ingetakiwa waambatane na viongozi wa mtaa ambao wangewathibitishia watuhumiwa kuwa hao ni polisi vilevile wananch wasingefanya fujo mbele ya viongoz wao ila hawa askari ambao wanajifanya wapo juu ya sheria wamevuna walichopanda, kwan raia walijua watakuwa ni majambazi ndo mana wakawashushia kipigo, polisi jifunzen kufuata sheria bila shuruti, pia nawapongeza wananchi wa sengerema kwa kujirinda dhid ya majambaz yanayojiita polis ni iman yangu hawa mambaz hawatarud tena na wakirud nagemea kuta taarifa ya polis waliokuwa wanafanya uharif wameuwawa na wananch wenye hasira kali
 

hahahaa! Hawa polis wetu hawa lolote yale huwa ni maigizo tu,ht wewe kwa mbinu ulizo nazo unawaacha polis mbali sn. Hawa polis wetu mbinu walizo nazo ni za kuomba rushwa nas kunyanyasa raia
 
Gongo inayotengenezwa na wazalendo inaonekana haram ila baa zetu zimejaa gongo tupu mfano ni gongo za viroba mbona zenyewe hawazikamati
 

hilo nalo neno, mtu anaweza kwenda kukamata lakini mamlaka za eneo hataki kuwahusiha, hii inaweza kujenga mzingira ya rushwa pia, na wanaogopa kuwahusisha mamlaka za mtaa kwa kuwa rushwa haitachukulika
 
ntagunga nimekuelewa, naku-regard kama miongoni mwa wahabarishaji wazuri!

Sikuchangia chochote kuhusu wanaharakati kwenye kadhia hii ya polisi kupigwa, lakini nikwambie sasa kuwa tukio hilo linalingana kwa maudhui kama si taathira, na maji kupanda mlima.

Tuwe na uelewa wa pamoja, Askari anapatiwa mafunzo mahsusi ya jinsi ya kutekeleza majukumu yake, kwa maneno mengine askari ni mtaalam wa saikolojia ya jamii angalau kwa mafunzo ya miezi 9.

Utaona wazi hapa polisi hakuwa mweledi vya kutosha ama alipuuza kwa maksudi au kwa msukumo wa kipato cha ziada, tahadhari ya "mob justice" ukijumlisha na maelezo yangu ya awali kuihusu gongo, utapata jawabu la hii "mob" ninayoi-refer kupambana na wanayemdhania kuwa mtunzi na mtia mkazo sheria wanayoiona kuwa kandamizi dhidi yao kwenye nyanja ya kiburudisho cha kilevi rahisi.

Ni kutokujitendea haki ikiwa tutadhani hili ni tukio la kupigiwa kelele na wanaharakati ambao wanauelewa wa kutosha kuhusu mamlaka, nguvu na wajibu walionao kisheria polisi wetu juu ya raia na mali zao.

Sisemi kuwa polisi wapigwe, la hasha, nasisitiza polisi kutumia taaluma yao preciously and positively.sheria na kanuni za kazi zizingatiwe, Kwa mfano ikitokea rabsha kwa wapenzi wa simba na yanga uwanja wa taifa, wakati simba inaongoza 4-0!!!!!!!!!! labda kamuhanda pekee ndiyo anaweza, lakini itakuwa ni kosa la mauaji kujaribu kutuliza rabsha hizo kwa mabomu ya mchozi kwenye uwanja uliofurika watazamaji zaidi ya 65,000. Likewise askari watatu kufanya jaribio la kukiarest kijiji kizima (hapa ni kwa mtizamo mpana) tegemea kuamsha jazba na munkari wa jamii husika.

Hapa uelewe hawa wananchi walikuwa wanafanya kama JWTZ ilivyofanya kwa idd amini alipovamia tanzania, ilikuwa kumpiga na kumtokomeza asionekane tena ili tishio lake litokomee pamoja naye,
walitaka huyu polisi asirudi tena au akome "kuwaonea" nimeutafsiri mtazamo wao.
 
Last edited by a moderator:
Unataka wanaharakati waseme nini? wanaharakati husemea wale wanyonge na pale haki inaposhindwa kupatikana lakini sasa hapa tayari watu waliotenda kosa washakamatwa na ninaamini hao Polisi watawashughulikia ipasavavyo................
 

jogi NAKUSHUKURU JOG KWA UCHAMBUZI WAKO NA NAMNA ULIVYOTAFSIRI MAAMUZI YA WANANCHI NA UKIMYA WA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU SUALA HILI. THANK YOU JOG
 
Unataka wanaharakati waseme nini? wanaharakati husemea wale wanyonge na pale haki inaposhindwa kupatikana lakini sasa hapa tayari watu waliotenda kosa washakamatwa na ninaamini hao Polisi watawashughulikia ipasavavyo................

HA HA HA......KWAMBA WATALIPIZA KISASI? NTAFUATILIA NIONE NINI KITAWAFIKA, NITAWAJUZA WADAU. LAKINI MIMI SIJAFURAHISHWA NA KUMPIGA MTU NUSRA YA KUFA. SIO FUNZO JEMA DA Elizabeth Dominic
 
imani na nyie polisi imepotea nawalaumu sana raia kwa kumuacha na uhai wangeua tu ,tulipie ile ya mwangosi,potelea mbali kila nikimuna polisi nashikwa na hasira yani kitendo chakugundua mleta mada ni polisi umeniharibia siku yangu,nikiwaona tu njiani natema mate chini laana kweli kweli hamwezi mkawa mnatumwa kama majini mnakwenda tu kama roboto,ninyamaze nsijekula ban bure mie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…