Askari polis sengerema, apigwa kipigo cha mwizi, Hali yake ni mbaya.

Maaskari Polisi hawahitaji mtu wa kuwatetea. Wana uwezo usio shaka wa kujitetea na kuwachukulia hatua wahalifu kwa misingi ya taratibu na sheria za nchi; fursa mara nyingi wanayoitumia si kwa manufaa ya taifa bali kwa sababu na maslahi yao binafsi. Wanaharakati ni sauti ya wanyonge, wenye kudhulumiwa ambao haki zao zinakanyagwa na mtu au kundi fulani na hawana uwezo wa kujitetea wala wa kuwakemea wanaowadhulumu. Narudia tena, tumesikia hadithi za upande mmoja na hatujasikia upande wa watuhumiwa kuwa ilikuwaje hadi tukio hilo kutokea. Nasisitiza tena; NI VIGUMU KUWAAMINI POLISI WA TANZANIA BILA YA KUPIMA WANACHOELEZA kutokana na tabia yao ya kugeuza ukweli, kutengeneza tuhuma (kubambikia kesi) dhidi ya raia wasio na hatia. Sisi tulioona yaliyotokea Arusha, na walioona yaliyotokea Morogoro, Songea na sehemu kadhaa wanaelewa ninachomaanisha. Hakuna wa kuziamini taarifa za polisi kwa asilimia mia moja siku hizi kabla ya kutafakari anachosimuliwa na polisi wetu hawa labda mwehu. Tunataka kusikia pia upande wa hao raia "walioasi" na kumwadhibu kiasi cha kutishia kuinyofoa roho ya mtumishi wao anayelipwa kwa kodi zao wenyewe.
 
Unaongelea uwajibikaji kwani akina Kamuhanda, Mwema, Jk, n.k n.k wamewajibika kwa makosa yao ya ufisadi na uchizi unaofanywa na Policcm?. Hao wananchi tena walikosea sana kama huyo jamaa hadi sasa hivi yupo hospital................ Siku zote dawa ya kiburi ni jeuri!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…