dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
Askari Polisi gani mwenye utu na Weredi kama ACP Theopista Mallya?
Shikamoo Afande
ACP Theopista Mallya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, naamini ni moja ya toleo bora la Askari Polisi tunaojivunia.
Aliwahi kuwa Msaidizi wa Mkuu wa Trafiki Tanzania Staff Officer Mnadhimu wa Polisi Makao Makuu.
Msikivu sana.. Si muongeaji sana bali Vitendo ndo vinaongea. Wakati nafuatilia kwanini hajateuliwa kuwa Mkuu wa Trafiki Tanzania baada ya Musilimu kuwa Kamanda wa Mkoa Morogoro sikupata jibu. Sababu kazi nyingi za Trafiki Tanzania alizifanya. Achilia mbali alipokuwa Makao Makuu ya Polisi.
Mtu alokuwa anatatua changomoto za Nchi nzima unampeleka kusimamia Mkoa mmoja? Alikuanadhimu wa Polisi Makao Makuu anadeal na Polisi Nchi nzima leo unampa asimamie Mkoa mmoja tena Rukwa. Na Rukwa alipelekwa kama kaimu akafanya kazi nzuri kama kawaida yake wakampa Ukamanda Mkuu. Sio kazi ndogo Polisi Mwanamke kufikia alipo na wote tunajua jeshi letu.
Alikuwa Msaidizi wa Mkuu wa Matrafiki Tanzania.
Sasa wakati nafuatilia kama kuna kitu kakosea au ana mapungufu gani hadi asipewe nafasi zinazomsitahili sioni. Hii ni kuharibu nguvu kazi kwa manufaa ya Wachache. Watoa Rushwa wanamchukia sana.
Ninachojua anachukia Rushwa.
Katika kumfuatilia mtandaoni nikakutana hili andiko linalomuelezea. Hili ni andiko la hawa jamaa RSA TANZANIA(Road Safety Ambassadors). Hawa ndo Jicho la Trafiki Tanzania sababu wametapakaa nchi nzima. Polisi na Madeva wa Tanzania nzima na wadau wa Usalama Barabarani. Wasome hapa ndo utamjua ACP Theopista Mallya japo kwa Uchache. Hakika anafaa kuwa mkuu wa Usalama Barabarani Tanzania. Sababu hawa wote watampa Ushirikiano. Wananchi wape wanachokitaka. Tanzania kwanza.
Hapa chini ni chapisho la May 20,2019 lilioandikwa na RSA TANZANIA.
KILA LA HERI AFANDE ACP T T Mallya KAMA STAFF OFFICER MPYA KINONDONI
Traffic Makao Makuu Uliitendea Haki.
Sijui mahala sahihi pa kuanzia, lakini naweza kusema kwa hakika kabisa kuwa katika watu waliowahi kutupatia ushirikiano mkubwa sana sisi RSA Tanzania katika hii kazi ya Usalama Barabarani basi ni wewe Mama yetu afande T.T. Mallya.
Kwamara ya kwanza nilikufahamu Geita wakati wa wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani. Nawe kwa wakti huo ndio kwanza ulikuwa umefika Kinondoni kama RTO. Katika siku ile nilipata kufanya presentation mbele ya RTOs kuhusu RSA. Wewe ni kati ya watu uliouliza maswali, lakini pia ulituomba jambo. Na hapa ninakumbuka ulisema hivi, “…RSA msaidie kuelimisha watu kuhusu matumizi ya daraja la kimara… Tangu wakati huu, haukuwahi kutuacha.
Na niseme kwa hakika kabisa hicho kiti ulichokuwa umekali hapo traffic kuu uliyeweka kuziba gepu lake tangu aondoke hapo afande SACP Johansen Kahatano, ni wewe.
Kati ya sifa zako na alama unazoziacha tutakazokukumbuka nazo ni:
1. Usikivu (listening)
Una uwezo mkubwa wa kumsikiliza mtu tena kwa utaratibu sana na kutoa hukumu au maamuzi
2. Umadhubuti (boldness)
Mtu akikusikiliza kwenye simu hizi tu au akukute unaomngea sehemu anaweza sema wee ni leissez faire, sana lakini ajaribu aone ndipo atagundua kuwa uko very firm. Haupendi mtu akutambuke tambuke hovyo. Kila anayedeal na wewe lazima ajue mipaka yake na amaintain hiyo mipaka.
3. Haki (fairness)
Siku zote umekuwa mtu wa kupenda kusimamia haki bila kujali kwamba anayehusika ni mtu anayekuhusu
4. Mwitikio wa haraka(quick response)
Wewe hata ukiwa likizo utapokea simu na kutoa maelekezo. Nakumbuka kuna wakati ulisema wambieni watu nipo likizo. Maana simu zilizidi. Lakini ulikuw amstahimilivu.
5. Ulitupenda(love)
Kwa sisi humu ndani wanarsa tunaweza kukiri bila shaka kabisa kwamba ulitupenda, na ndio maana hujawahi kutoka humu, lakini pia hata sometimes tulikuwa tunajoke humu. Na upendo huu umzidi kujidhirisha kwa kutuaga.
6. *Urasimu*bureaucracy)
Japokuwa urasimu ni sehemu muhimu ya uendeshaji wa ofisi, urasimu nao ukizidi sana huzorotesha kazi(inefficiency). Wewe hukuwa na urasimu uio na sababu.
7. Weledi (Professionalism)
Mama hakika kichwani uko njema tu, unao uwezo wa kudapta haraka sana kulingana na mazingira na wakati. Yaani hata ungepelekwa kikosi gani sasa hivi, naamini utafanya vema tu sababu una-uwezo mkubwa sana wa kuadopt. Charles Darwin aliweka nadharia ya surivival of the fittest, lakini Herbet Spencer akaongeza kwamba * It Is Not the Strongest of the Species that Survives But the Most Adaptable. Nami nakuweka katika kundi la the most adaptable.
Kila la heri mama yetu, dada yetu afande T.T. Mallya katika majukumu yako mapya. Pale tulipokwazana tusameheane. Nasi tunakuahisi kuendelea kushirikiana na wewe kokote utakakokuwa. Tunamsubiri yeye ajaye ili tushirikiane naye huku tukiamini ataendeleza ushirikiano.
RSAadmin1
RSA Tanzania.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.
Mwisho.
Theopista Mallya ndo Mkuu wa Trafiki ajaye.