Nijuavyo mimi JWTZ ukiwa na degree enzi zetu ulikuwa unaenda moja kwa moja Cadet,Ukitoka cadet unarudi na nyota moja(Luteni usu), baada ya muda unapata mbili luteni, kwa madaktari walikuwa wanaanzia Major kuendelea.
Kwa upande wa Polisi ndio sijui rank zao zikoje huko ndio maana nikasema kama unauelewa msaidie.
Hapa humuoni huwezi jua anaweza kunyenyekea akakushangaza.
Mimi nilikuwa siwezi kabisa kumyenyekea mtu, nilikuwa mtukutu sana tangu utotoni, lakini nilishangaa ukubwani nilijifunza kunyenyekea, kwa sababu kwenye maisha unaweza ukajifanya mjinga kwa muda mfupi yanapiata na ukaendelea na kiburi chako huko uendako.
Mpe shule unaweza kumsaidia kwa namna usiyoweza kuijua.