Askari polisi wakamatwa na meno ya tembo Serengeti

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Posts
1,002
Reaction score
277
Ni tukio lililotokea leo mjini Mugumu wilayani Serengeti na kuthibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Mara Absalom Mwakyoma.Askari hao ni Koplo David Delina mwenye namba E9172 kutoka ofisi ya upelelezi makosa ya jinai kutoka Biharamulo na mwenzake Gerlad Tuti mwenye namba F5553 kutoka ofisi ya upelelezi makosa ya jinai Bukoba na raia aitwaye Boniface Kurwa mwenyeji wa Geita.
Source:mdau wangu anayefanya kazi kituoni hapo.
 
Duh !!
Hii zaidi ya kali
MUNGU ibariki Tanzania

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Duuu Mlinzi Mwizi,Askari Mwizi na tulimkabidhi dhamana ya mali naye mwizi tumkabidhi nani tena? Hv msomali hausiki kweli hapa? Maana alishawahi safirisha contena la meno ya tembo!!
 
Haya yanaweza tokea Tanzania pekee, Hata kule Somalia kwenye Vita huwezi kuta madudu kama haya
 
hizo ni moja ya kazi zao, labda walitumwa na wale wa juu yao.
 
Huenda ni utekelezaji wa ilani, "maisha bora kwa kila mtanzania"
 
Tangu ufisadi uwe sera ya taifa sioni tofauti ya majambazi na askari matapeli na watawala nk. Usishangae wakafutiwa kesi kwa kukosa ushahidi ikizingatiwa kuwa watakaofanya upelelezi na kutunza vielelezo ni majambazi wenzao waliovaa magwanda.
Ni tukio lililotokea leo mjini Mugumu wilayani Serengeti na kuthibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Mara Absalom Mwakyoma.Askari hao ni Koplo David Delina mwenye namba E9172 kutoka ofisi ya upelelezi makosa ya jinai kutoka Biharamulo na mwenzake Gerlad Tuti mwenye namba F5553 kutoka ofisi ya upelelezi makosa ya jinai Bukoba na raia aitwaye Boniface Kurwa mwenyeji wa Geita.
Source:mdau wangu anayefanya kazi kituoni hapo.
 
Ni tukio lililotokea leo mjini Mugumu wilayani Serengeti na kuthibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Mara Absalom Mwakyoma.Askari hao ni Koplo David Delina mwenye namba E9172 kutoka ofisi ya upelelezi makosa ya jinai kutoka Biharamulo na mwenzake Gerlad Tuti mwenye namba F5553 kutoka ofisi ya upelelezi makosa ya jinai Bukoba na raia aitwaye Boniface Kurwa mwenyeji wa Geita.
Source:mdau wangu anayefanya kazi kituoni hapo.
Aisee hiri Kopro Delina ndio linamiliki Yale magari ya kifahari yalioandikwa DELINA kwenye number plates!? Kuuliza si ujinga wajameni.
 
Back
Top Bottom