Askari waliovalia sare za Jeshi la Polisi wameweka ulinzi mkali katika Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Nyumba ya Ufufuo na Uzima), eneo la Ubungo Dar es salaam huku njia zote zinazowezesha Watu kufika kwenye kanisa hilo zikiwa zimezuiwa.

Ikumbukwe Juni 13, 2025, Naibu Katibu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, Askofu Maximilian Machumu β€œMwanamapinduzi” amesema taarifa kuwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa amefungia Kanisa lao, si za kweli bali lililofungiwa ni Kanisa la Glory of Christ Church ambalo halina uhusiano na Kanisa lao, hivyo Jumapili hii wanatarajia kurejea Kanisani kuendelea na Ibada.

Baadhi ya waamini wamejitokeza maeneo ya karibu na Kanisa hilo lililopo Ubungo.





​

Pia soma:
~
Askofu Machumu wa Gwajima asema Kanisa lao halijafungwa, waapa kurejea kanisani Jumapili
~ Kanisa la Mwanamapinduzi Kibaha lawekwa utepe, waumini wafukuzwa
~ Dar: Mahakama ya Kisutu yajiweka kando kutoa uamuzi kesi ya Dkt. Slaa, Hakimu adai anafungwa mikono na Rufaa ya Jamhuri
 
UHURU WA KUABUDU UNATOWEKA TARATIBU

KILICHOBAKI NI KUTANGAZWA KUWA ISLAMIC STATE
 
Jeshi la Polisi katika mkoa wa Pwani limeimarisha ulinzi katika Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church.

Katika kanisa hilo wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani linaloongozwa na Askofu Maximilian Mahumu maarufu Mwanamapinduzi, magari ya polisi yamefika yakiwa yamejaa askari na kuzingira kanisa hilo.

Itakumbukwa Juni 13, Mwanamapinduzi aliwaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa kanisa hilo halijafungiwa hivyo leo watasali kama kawaida.

Hata hivyo, Juni 14, watu waliovaa sare za polisi walifika na kuweka utepe kuzunguka kanisa hilo.
Akizungumza leo na Jamii Forums, Askofu Mwanamapinduzi amesema; "tutasali hata nje ya utepe, haki yetu ya kuabudu iko pale pale."



​
 
Vp kaashafika kuswalisha ama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…