Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Asubuhi na jioni ni muda ambao magari huwa mengi na askari wa usalama barabarani(Traffic) hujitahidi kupunguza adha hii kwa kuzipa kipaumbele barabara ambazo zina msongamano mkubwa zaidi wa magari.
Kinachotokea, mathalan upo kwenye barabara yenye magari pungufu, askari huyo ukakuzuia na ukawa mbele karibu na taa unaweza kulazimika kusubiri dakika 20 Traffic awajaze kwanza foleni ndio awaruhusu kwa pamoja, ratio yake ya kuruhusu ikawa dakika 20 kwenye msongamano kwa dakika 5 kusipo na msongamano(20:5), ukiwa kwenye msongamano unaweza kupita haraka zaidi na barabara iliyo nyeupe ukalaani traffic mpaka laana zikaisha.
Askari huyu wa Morocco pia anatoa muda mwingi zaidi kwa barabara yenye msongamano(Mwenge-Mjini) lakini anavunja kwenye makundi zile dakika nyingi kutowaweka watu, mfano badala ya kuwa 20:5 inakuwa 5:1. Kila baada ya dakika 5, anaziondoa gari chache zilizo kwenye barabara isiyo na kipaumbele, trafffic wengine unaombea uwe kwenye barabara yenye msongamano ili upite haraka kuliko kugandishwa kwenye barabara zisizo na magari mengi, yani anaweza kuita magari ambayo hayaonekani kutoka barabara kubwa.