KERO Askari wa Jangwani wanaokamata Bajaj wawe na lugha ya staha!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wale Askari wapale Jangwani wanaokamata usafiri kama Bajaj wawe na kauli nzuri na ustaarabu kwa abiria walioko ndani ya usafiri.

Wanawafanya watu kama wezi na kuwatolea maneno machafu na kufanya kazi kwa kujuana, imekuwa kero, yaani wanakamata Bajaj kisha wanaanza kutoa lugha isiyo ya kiungwana kwa watu wote waliopanda, wanadhani wanavyowafokea madereva na wengine pia tunaona nis awa kuvumilia ujinga wao!
 
Kwa polisi wetu walio wengi kuwategemea wawe waungwana ni sawa na kutegemea mbuzi wacheze wanapopigiwa muziki!
 
Askari akikamata Bajaji abiria anahusikaje?
Kwanini atolewe lugha chafu?
Ni lugha gani hizo?
 
Usikute huwa mnaanza kuleta ujuaji, yan polisi akate bajaji aanze kutukana abiria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…