Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mhhhh! mgambo nao wanapewa rugu sasa kufanya wanachoweza na hivi hawa jamaa wanapenda sifa tutayaona mengi. Maana nakumbuka mama ntile walivyokuwa wanapata shida kutoka kwa mgambo na kumwangiwa vyakula vyao ni shida
=================
Zaidi ya askari 290 wa Jeshi la Akiba waliomaliza mafunzo wilayani Babati, mkoani Manyara, wametakiwa kuhakikisha wanaimarisha amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu, huku wakikumbushwa kuepuka matumizi mabaya ya mafunzo hayo kwani ni kinyume cha sheria.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo yaliyofanyika kata ya Mamire, Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda amesema Serikali inatarajia wahitimu hao kutumia ujuzi walioupata kulinda wananchi na kudumisha mshikamano wa kitaifa.
Naye Mshauri wa Jeshi la Akiba wilayani Babati, Kulwa Machupa, amewataka wahitimu hao kuwa mfano wa uadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa ambavyo vinaweza kudhoofisha heshima na dhamana waliyopewa.