Askari wa Kizulu Katika Jeshi la Wajerumani Tanganyika 1890s - 1914

Askari wa Kizulu Katika Jeshi la Wajerumani Tanganyika 1890s - 1914

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ASKARI WAZULU KATIKA JESHI LA WAJERUMANI 1890s - 1914
Kwa miaka mingi bila mafanikio nimekuwa nikitafuta picha ambayo inaonyesha askari mamluki waliokwenda kuchukuliwa Mozambique na Hermann von Wissmann kuja German Ostafrika kama Tanganyika ilivyokuwa ikijulikana kuja kupigana na Bushiri Al Harith na Mtwa Mkwawa.

Leo nimeipata picha hiyo hapo chini kutoka kumbukumbu za Tom von Prince afisa katika jeshi la Wajerumani aliyeshiriki katika vita hivi na nimeiweka hapa sote tuione.

(Huyu Tom Prince ndiye Mjerumani aliyemsaidia Chief Merere dhidi ya Mkwawa.
Kalenga Museum kuna barua aliyoandika Mtwa Mkwawa kwa hati za Kiarabu na ndani ya barua hii Mkwawa anaeleza usaliti wa Chief Merere wa Usangu.

Mkwawa alisilimishwa Abushiri bin Salim akawa Muislam na jina alilochagua ni Abdallah na Abushiri ndiye aliyemfunza kusoma na kuandika).

Pamoja na picha hii ya hawa askari Wazulu naweka maelezo kidogo:

''Efffendi Plantan, Sykes Mbuwane na mamluki wengine wa Kizulu walikuja Tanganyika katika meli ya kivita ya Wajerumani ikitokea Laurenco Marques iliyotia nanga Pangani mwaka 1894.

Wazulu hawa walitokea Inhambane, Msumbiji iliyokuwa ikitawaliwa na Wareno.
Kijiji chao kilikuwa kinajulikana kama Kwa Likunyi. Mjerumani alIyewaleta toka huko alikuwa na sifa ya kuwa mwanajeshi na mvumbuzi, Harmine von Wissman.
Wazulu wenyewe walikuwa wakiwaeleza watoto wao kuwa:

‘’Wajerumani waliweka mkataba na Mohosh, Chifu wa Inhambane nchini Msumbiji, kuwa watu wake watakwenda na Wajerumani hadi Tanganyika kupigana, wakakubliana kuwa ardhi yoyote watakayoteka watagawana sawasawa kati ya Wazulu na Wajerumani.

Wajerumani waliwachukua Wazulu katika meli hadi Pangani chini ya uongozi wa Mohosh, shujaa wa vita ambaye baadae alikuja kujulikana kwa jina la Effendi Plantan.’’

Kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998)

Huyu Affande Plantan ndiye baba yao Thomas Saudtz Plantan, Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan na hawa wote walizaliwa Mozambique walikuja German Ostafrika wakiwa wakubwa.

Mtoto wa mwisho kuingia nchini alikuwa Mashado Plantan mwaka wa 1905.
Affande Plantan ndiye babu yake Bi. Maunda Plantan, mwalimu wa shule na mtangazaji wa kwanza mwanamke Sauti ya Dar es Salaam ilipoanzishwa mwaka wa 1952 na alikuwa English Service.

Kitu kitakachokushtua kwa haraka ukizungumza na Bi. Maunda ni ule ulimi wake katika kuzungumza Kiingereza.

Hali kadhalika baba yake mzazi Thomas Plantan alikuwa akizungumza Kijerumani fasaha kabisa na wakiizungumza lughs hii wakati wa utawala wa Waingereza.

Nimepata kuweka video ya Thomas Plantan akizungumza Kijerumani katika kumbukumbu ya kifo cha Paul von Lettow Vorbeck ambae alikuwa Mkuu wa Majeshi ya Ujerumani Tanganyika Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918).

Ukoo wa Plantan una historia kubwa katika siasa za African Association, TAA, Al Jamiatul Islamiyya na TANU.

Schneider Plantan yeye alikuwa Secretary wa Daawat Islamiyya taasisi ya Kiislam iliyokuwa ikiongozwa na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na ndiye aliyeongoza mapinduzi baridi kumtoa kaka yake, Thomas Plantan katika uongozi wa TAA na kuingiza uongozi wa vijana Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi mwaka wa 1950.

Mashado Plantan alikuwa muhariri wa gazeti lake mwenyewe Zuhura.
Picha: Askari Wazulu, kitabu chenye kumbukumbu ya Tom von Prince na barua ya Mkwawa kwa Chief Merere.

1659125976410.png

1659125938570.png

1659125716245.png
 
Hii Tanganyika kabla ya kuitwa German Ostiafrica je ilikuwa ikiitwaje?

Nina hamu tupate history kurudi nyuma zaidi.
 
Hii Tanganyika kabla ya kuitwa German Ostiafrica je ilikuwa ikiitwaje?

Nina hamu tupate history kurudi nyuma zaidi.
Matola,
Tanganyika ilikuja baada ya Waingereza kuchukua nchi waliposhinda WWII 1914 -1918.
 
Matola,
Tanganyika ilikuja baada ya Waingereza kuchukua nchi waliposhinda WWII 2014 -2018.
Ingawa umekosea kuandika hiyo miaka hapo si kitu ni makosa ya kiuandishi tu.

Swali langu ni kabla ya German Ostiafrica, nchi yetu bara ilikuwa inaitwaje? au hakukuwa na nchi bali kila Chifu na nchi yake kwenye kabila lake.

Hapa historia iko kimya wengi tupo gizani, tunafundishwa tu historia ya kuanzia miaka ya 1800 tu, ya missionaries, explorer and traders.
 
Tanganyika ilipatikana baada ya Berlin conference, kabla ya hapo kulikuwa na vichiefdom viiiingi
 
Uzee na changamoto zake
Ahsante.
 
Berlin conference ilikuwa mwaka 1884 kwahiyo hapa jina la German Ostiafrica lilikuwa bado?
German ostafrica Wala haikuwa nchi , ni jina la kampuni iliyokuwa inasimamia eneo lote kuanzia pwani hadi rwanda urundi

Baada ya Berlin conference kuweka mipaka Ili mabeberu wasigombane ndipo ikapatikana Tanganyika
 
Kwahiyo upo ukweli dola la watu weusi yani Zanzibar lilikuwa linamiliki na ardhi kubwa tu upande wa bara hasa pwani ya Indian ocean?
 
Kitu kitakachokushtua kwa haraka ukizungumza na Bi. Maunda ni ule ulimi wake katika kuzungumza Kiingereza.

Hali kadhalika baba yake mzazi Thomas Plantan alikuwa akizungumza Kijerumani fasaha kabisa na wakiizungumza lughs hii wakati wa utawala wa Waingereza.

Nimepata kuweka video ya Thomas Plantan akizungumza Kijerumani katika kumbukumbu ya kifo cha Paul von Lettow Vorbeck ambae alikuwa Mkuu wa Majeshi ya Ujerumani Tanganyika Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918).
Mkuu,
Kama una clip tuwekee hapa basi!
 
German ostafrica Wala haikuwa nchi , ni jina la kampuni iliyokuwa inasimamia eneo lote kuanzia pwani hadi rwanda urundi

Baada ya Berlin conference kuweka mipaka Ili mabeberu wasigombane ndipo ikapatikana Tanganyika
Sendoro...
Angalia Google:

German East Africa (German: Deutsch-Ostafrika) (GEA) was a German colony in the African Great Lakes region, which included present-day Burundi, Rwanda, the Tanzania mainland, and the Kionga Triangle, a small region later incorporated into Mozambique. GEA's area was 994,996 km2 (384,170 sq mi),[2][3] which was nearly three times the area of present-day Germany, and double the area of metropolitan Germany then.

The colony was organised when the German military was asked in the late 1880s to put down a revolt against the activities of the German East Africa Company. It ended with Imperial Germany's defeat in World War I. Ultimately, GEA was divided between Britain, Belgium and Portugal and was reorganised as a mandate of the League of Nations.
 
German ostafrica Wala haikuwa nchi , ni jina la kampuni iliyokuwa inasimamia eneo lote kuanzia pwani hadi rwanda urundi

Baada ya Berlin conference kuweka mipaka Ili mabeberu wasigombane ndipo ikapatikana Tanganyika
Nadhani hiyo unayoisema iliitwa IGEACO(Imperial German East Africa Company) ambayo ilikuwa na kazi ya kuhakikisha Ujerumani inakamata makoloni katika ukanda wa Afrika Mashariki.Wale Waingereza walikuwa na IBEACO(Imperial British East Africa Company).
 
Tanganyika ilipatikana baada ya Berlin conference, kabla ya hapo kulikuwa na vichiefdom viiiingi
Berlin conference haikutengeneza Tanganyika,Tanganyika iliundwa baada vita ya kwanza ya Dunia wababe walipokaa pale Verssailes nakuja na mkataba ambao,pamoja na mambo mengi e ,waliamua kugawana yalokuwa makoloni ya Ujeruman.Hapo ndipo German East Africa ikazaa,Burundi,Rwanda na iliyokuja kuitwa Tanganyika.Mbili za kwanza alipewa Mbelgiji ambaye akitawala Kongo ya chini na iliyokuja kuitwa Tanganyika alipewa Muingereza.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom