Askari wa Misenyi wamefukuzwa kazi kwa kosa gani na sheria gani?

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
wale askari waliopiga picha wakiwa kwenye nahaba mazito wamefukzwa kazi sasa swali
1.kwa kosa gani nakwa sheria gani
2.na aliyewapia naye ana kosa gani na kwa sheria gani
3.je askari anaruhusiwa kuvuta sigara ua kunywa pombe akiwa kwenye sare za jeshi

wataalamu karibuni mnisaidie
 
nakunywa chai alafu nitarudi kuja kukufafanulia mkuu.. ila adhabu waliyopewa iko sawa kabisaaa
 
Katika utumishi wa umma kuna ethics zinaotakiwa kufuatwa ukizikiuka unaadhihiwa kwa mujibu wa kanuni za maadili na utumishi ukiukwaji wa kanuni za maadili adhabu yake ni kufukuzwa kazini iwapo askari hao walifanya hivyo na kama taratibu za kuwafukuza kazi zilifuatwa hao askari adhabu waliyopewa ndiyo stahili yao
 
wale wawili sawa aliyewaphotoa je ana kosa gani?na sura zao pia hazionekani vizuri wala namba zao za upolisi hazionekani vizuri isije kuwa wameonewa
 
Mimi si mwanasheria, ila ukisoma sheria ya ajira na mahusiano kazini, sura ya kwanza inasema:
2.-(1) Sheria hii itatumika kwa wafanyakazi wote ikiwa ni pamoja na wale wa utumishi wa umma wa Serikali ya Tanzania wa Tanzania Bara, lakini haitatumika kwa wajumbe, wawe ni wa kudumu au wa muda katika ajira kwenye: - (i) Jeshi la Wananchi la Tanzania ; (ii) Jeshi la Polisi; (iii) Jeshi la Magereza; (iv) au Jeshi la Kujenga Taifa.
Sasa yamkini wana sheria zao.
 
matege hiyo chai umealikwa na jk ikulu nini haiishi nasuburi umwage nondo hapa

nchi inaongozwa na katiba ila kila institution au organisation ina by laws inayoziongoza ila tu zisikiuke Katiba ya nchi ambayo ndo sheria mama. Jeshi la Polisi linaongozwa na Police Force Service Regulation Act (PFSR). mtumishi yeyote wa jeshi la polisi anatakiwa kufuata sheria hizo na failure to do so basi adhabu yake ni dismissal from the force. mkuu niko kwny movement ila nikifika home nitarudi kuelezea hili mkuu.
 
Vijana nendeni Jkt mtajua ethics za vyombo vya ulinzi na usalama.
 

Asante mkuu, jibu muafaka kabisa!
 
walistahili kupewa onyo kwanza ni mtazamo tu kwani tech iko juu sana kwani kuna baadhi ya web site zimefungwa kwa sababu yaa adv of tech. na matumiz mabaya na kupost vtu vsivyo faa.
 
walistahili kupewa onyo kwanza ni mtazamo tu kwani tech iko juu sana kwani kuna baadhi ya web site zimefungwa kwa sababu yaa adv of tech. na matumiz mabaya na kupost vtu vsivyo faa.
kabisa mkuu onyo au mmoja angepelekwa mtwara yaani sio kama nawatetea ila kuna makosa makubwa polisi wanayafanya kama mauaji ya raia wema hawafukuzwi badala yake wanapandishwa vyeo,kapicha tu imekuwa nongwa
 
Walistahili kupata adhabu hii na kupelekwa mahakamani kwa kuidhalilisha jamii ya kitanzania,
swali pia linakuja hawa ni wanandoa huko nyumbani?
 
Nadhani suala hili tukiliangalia kwa mapana sana tutakubaliana kuwa huo ndio uwajbikaji wa viongozi wa sasa tunao wahitaji kwaajili ya maendeleo ya Taifa letu,nikimaanisha kuwa kila mmoja awajibike kutokana na position yake kama kamanda wapolisi mkoan Kagera alivyo wajibika kwa kuwafukuza kazi kwa kukiuka maadili ya jeshi la polisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…