A
Anonymous
Guest
Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa (Sumbawanga) kuna changamoto kwa Askari Polisi wa doria. Wanatumia mamlaka yao vibaya kutunyanyasa vijana, wanatupokonya simu zetu bila kuwa na sababu za msingi.
Iko hivi: Hawa Askari wa doria wakipita sehemu ambapo kuna mkusanyiko wa watu wengi au wachache, sanasana vijana, wanatuamuru kutoa simu zetu, password na kuanza kukagua, na kukutaka uoneshe risiti ya uliponunulia simu hiyo. Kama huna, wanaichukua simu, au kama laini inayotumika katika simu hiyo usajili wake sio wa majina yako, wanaichukua pia.
Na wanadai pesa kubwa sana ili uweze kurejeshewa simu yako, na kama huna pesa, simu ndio hairejeshwi. Hii imekuwa ni kero ya muda mrefu sana.
Wanapokuja hawajitambulishi kama taratibu zinavyowataka kufanya. Maana hadi mbishane kwa muda mrefu ndio wanatoa kitambulisho kuonesha kwamba wao ni Askari. Lakini je, swali la msingi, mamlaka hayo ya kuchukua simu zetu wanapata wapi?