Askari wa usalama barabarani mnasababisha foleni acheni taa ziongoze magari

Askari wa usalama barabarani mnasababisha foleni acheni taa ziongoze magari

Doctor Ngariba

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2020
Posts
588
Reaction score
951
Ladies and Gentlemen nawasalimu kwa "Amani ya Muumba iwe nanyi"

Nikiri kuwa kuna mambo yanaenda sivyo ndivyo tangu Nzilankende arest in peace kwa mfano ukataji wa umeme hovyohovyo. Pia mengine yanaenda shwari.Hebu kila mmoja atimize wajibu wake.

Niende moja kwa moja kwenye mada, Ni kwamba kumekua na foleni za magari barabarani zinazosababishwa na askari wetu wa usalama barabarani kitu ambacho hakikuwepo kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita.

Nachelea kusema kwamba kuna hujuma dhidi ya chief Hangaya hata hivyo kuna dalili flani ya dharau na uzembe unaofanywa na baadhi ya askari wetu tajwa.

Kwa joto lililopo Dsm kwa sasa nawaombeni muziache taa ziongoze magari au nyie mapoti mutumike kwa uchache na ikibidi tu kwenye zoezi la kuongoza magari na isiwe daily routine kwenu.

Nimalizie kwa kuheshimu baadhi ya elements za UDICTATOR kwani kwa hali ilivyo inaonesha bila ubabe baadhi ya viongozi hawawezi kufanya chochote chenye maana na kinyume chake wanadeal na vitu petty kama kumshikilia Mbowe na vingine.

Samahani,
Hivi ni kweli tunaelekea kuwa na deficit ya mafuta?!!! Na huu umeme nao si Makamba alibadilisha board?!!
Nakupenda rais Wangu mama SSH,
Magufuli kuna pahala utakumbukwa kwa maamuzi magumu.
 
Back
Top Bottom